Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atatuma mkaguzi aende
kuchunguza hali ya upatikanaji wa dawa kwenye zahanati na kituo cha afya cha
mjini Gairo, mkoani Morogoro.
Ametoa ahadi hiyo, wakati akiwahutubia wakazi wa mji wa
Gairo na vitongoji vyake kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja
vya shule ya msingi Gairo ‘A’.
Waziri Mkuu alifikia uamuzi huo baada ya kumhoji Mganga Mkuu
wa Wilaya hiyo, Dk Albert Lyaruu kama anamiliki duka la dawa au la na kujibiwa
kwamba hana duka la dawa. Lakini pia Dk. Lyaruu alikiri kwamba baadhi ya
watumishi wa idara yake wanayo maduka ya dawa.
Sasa ni lazima nilete mkaguzi kutoka ofisi yangu ili tupate
picha halisi kama dawa zinazoletwa zinafika, na kama zinafika zinatumikaje.
Huyu mkaguzi atakuja kukukagua wewe mwenyewe na kwenye zahanati zako,” amesema
Waziri Mkuu
Kwenye mkutano wangu na watumishi wa Serikali nimewaeleza
kwamba ninyi ni desk officers (maafisa wa kukaa ofisini tu), wala hamuendi
vijijini kuona hali halisi ikoje. Ndiyo maana wananchi hawa wanalalamikia
kukosa dawa na wewe wala hujui,” amesema
Ni lazima uende kwenye vituo vya afya na zahanati na ucheki
matumizi ya dawa la sivyo unaweza kupata kesi kama ya Shinyanga ambapo mganga
wa kituo cha afya alikutwa na dawa za Serikali nyumbani kwake, baada ya wanachi
kumwekea mtego hadi akakamatwa
Serikali haizuii watumishi kuwa na maduka ya dawa,
tunachokataa sisi ni kuchukua dawa za Serikali ambazo zinatakiwa kuwatibu
wananchi na kuzipeleka kwenye maduka yenu. Tumezuia pia kuwepo kwa maduka ya
watu binafsi nje ya hospitali, zahanati au kituo cha afya,” amesisitiza
Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa Gairo wawe macho na
walinde mali za umma na inapobidi watoe taarifa mara tu wanapobaini kuna mtu
anatumia mali ya umma vibaya
Waziri Mkuu alikuwa amemwita jukwaani, Dk. Lyaruu ili aeleze
ni kiasi gani cha fedha amepokea kutoka Serikalini kwa ajili ya ununuzi wa
dawa. Alipotoa mchanganuo wake, wananchi waliohudhuria mkutano huo walizomea na
kudai kuwa siyo kweli
Ninapokea Sh 109 milioni kila robo mwaka. Na katika kipindi
cha miezi mitatu ya mwisho tumepokea Sh 109 milioni na kati ya hizo tunatoa
asilimia 33 ambazo ni sawa na Sh 36 milioni kununua dawa na vifaa tiba. Kwa
hiyo hadi sasa hali ya dawa ni nzuri na upatikanaji wake ni kati ya asilimia 85
hadi 90,” amesema Dk Lyaruu
Kutokana na majibu yake hayo, wananchi walimzomea daktari
huyo na kudai kuwa wananunua dawa hizo kwenye maduka ya dawa. “Tunanunua Waziri
Mkuu,” walisikika wakisema
Hata hivyo, Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi
waliohudhuria mkutano huo kwamba dawa zinazopatikana kwenye zahanati
zinatofautiana na dawa zinazopelekwa kwenye kituo cha afya, hospitali ya wilaya
au ya mkoa. Wilaya ya Gairo haina hospitali ya wilaya
Waziri Mkuu atuma mkaguzi kituo cha afya Gairo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment