Wananchi wa Kitongoji cha Bujinge,kijiji cha Nhelegani kata
ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya
kuchimba kaburi kisha kulazimika kufukia kaburi hilo la mtoto aliyedaiwa
kufariki dunia.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo,Salum Juma,amesema kuwa
mama mmoja Suzana
Charles aliekuwa ameolewa huko
Musoma,aliondoka Shinyanga akiwa na mtoto aliyezaa na mwanamme mwingine,lakini
badae akapiga simu nyumbani kwao Kizumbi kuwa mtoto wake amefariki,na
wanasafirisha mwili wa marehemu kutoka Musoma hadi Shinyanga.
“Jana tulihudhuria msibani nyumbani
kwa marehemu Mzee Charles hapa Kizumbi,tukachimba kaburi,tukawa tunawasiliana
naye akisema wapo njiani wanakuja,baadaye huyo mama akasema wamefika Misungwi
Mwanza lakini gari yao imemaliza mafuta hivyo tuwatumie pesa,tukawatumia
shilingi laki moja na simu yake haikuwa inapatikana tena”,anasimulia Juma.
“Baada ya kutuma shilingi laki
moja,tukategemea kuwa safari inaendelea,tukaendelea na taratibu za mazishi
tukiamiani kuwa mpaka saa tisa alasiri watakuwa wamefika Shinyanga,huwezi amini
mpaka saa 12 walikuwa bado hawajafika,tukakubaliana kuwa kesho yake yaani leo
tufike kwa ajili ya kuendelea na msiba”,
“Ilipofika saa nne usiku
jana,Yule bwana aliyekuwa amemuoa huyo mwanamke akapiga simu anauliza mke wake
kama amefika Shinyanga? Maana ametoka Musoma,tukamuuliza kuhusu msiba,akasema
hana taarifa za msiba kwani mke wake ametoroka na mtoto akiwa salama”,
“Leo tumeamka tukaambiwa kuwa
hakuna msiba wowote,hivyo nzengo tumedanganywa,na kaburi letu tulikuwa
hatujalifukia tunaendelea kujadili,kidogo majira ya saa nne asubuhi leo
Jumapili Yule mama akawa amewasili Kizumbi,Shinyanga akiwa na mwanae,amefika
hapa kwao,tumempokea,tukaanza kumhoji kuhusu kilichotokea”,
“Tulipomhoji amesema ameamua
kufanya hivyo kutokana na matatizo ya kifamilia kule alikokuwa anasumbuliwa na
maradhi hana pesa ya kumsaidia kupata matibabu,imefikia hivyo na sasa ndiyo
tumemaliza kufukia kaburi”,anaeleza Salum Juma.
WANAKIJIJI WATANGAZIWA MSIBA FEKI SHINYANGA, WACHIMBA KISHA KUFUKIA KABURI LA MTU ALIYE HAI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment