Wawili wapoteza maisha ajali ya trekta



Watu wawili wamefariki dunia na wengine 29 wamejeruhiwa baada ya tela la trekta walilokuwa wamepanda kutoka kitongoji cha Lorngoswani kwenda Kijiji cha Terrat Wilayani Simanjiro, Manyara kupata ajali na kupinduka

Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula akizungumza kwa njia ya simu amesema tukio hilo limetokea leo jumapili saa tatu asubuhi karibu na Kijiji cha Terrat

Amesema watu hao walikuwa wakienda kwenye tamasha la kwaya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Mhandisi Chaula amesema wanawake wawili walikufa papo hapo katika ajali hiyo, watu 29 wakiwemo watoto wadogo wawili walikimbizwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru.

Majeruhi wenine 15 walitibiwa kwenye zahanati ya Terrat lakin nao baadaye walikimbizwa Mount Meru baada ya hali zao kuwa mbaya.

Amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana mara moja ila polisi wameshafika eneo la tukio kwa uchunguzi zaidi.


Wawili wapoteza maisha ajali ya trekta Wawili wapoteza maisha ajali ya trekta Reviewed by KUSAGANEWS on June 04, 2017 Rating: 5

No comments: