WATANZANIA WACHACHE WAJITOKEZA KUTEMBELEA BURE HIFADHI ZA TAIFA



Watanzania wachache wamejitokeza kuingia bure kutalii katika hifadhi za Taifa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) kutokana na ofa iliyotolewa na serikali.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika lango la kuingia Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, baadhi ya watanzania waliojitokeza kutembelea hifadhi, walieleza wamefurahishwa na ofa ya serikali kutebelea bure hifadhi kuanzia jana  hadi june 4 mwaka huu.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais( Mazingira), Januari Makamba kwa kushirikiana na wizara ya Maliasili na Utalii, walitangaza ofa hiyo mapema wiki hii, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya mazingira na pia kuhamasisha uhifadhi na utalii wa ndani.

Veneranda Mgoba alisema ameamua kuitumia ofa hiyo ya serikali, kutembelea hifadhi ya Ngorongoro, ambayo ina vivutio vingi ikiwepo creta, wanyama wa aina mbali mbali kama Faru, Tembo na Simba ambao rahisi kuonekana kuliko hifadhi yoyote nchini.

Naamini Jonas alisema amefurahi kutumia fursa ya kuingia bure hifadhini na akatoa wito kwa watanzania wengine kutumia fursa hiyo kikamilifu kwani ni jambo jema sana kutalii.

Wakizungumzia kujitokeza watazania wachache, Meneja uhusiano wa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro, Vicent Mbilika na Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Manyara, Dk Noelia Myonga walisema ingawa jana walijitokeza watu wachache wanaamini leo na kesho wataongezeka.

Mbilika alisema waamini jana kwa kwa ni siku ya kazi, wafanyakazi wengi walikuwa makazini, lakini leo na kesho watatembelea hifadhi ili kujionea utajiri wa rasilimali walizonazo watanzania.

"naimani watanzania wakifika Ngorongoro watajua umuhimu wa uhifadhi wa mazingira na pia kutembelea vivutio vya utalii kwani kuna mambo mengi ya kujifunza kuhusu wanyama wa aina mbali mbali na mazingira yao"alisema

Alisema pa katika hifadhi hiyo kunapatikana historia ya binaadamu, kutokana na  kuwepo masalia ya zamadamu wa kale na eneo lenye nyayo za Zamadamu na maeneo mengine ya kuvutia kama mchanga ambao unatembea.

Kwa upande wake Dk Myonga alisema siku ya kwanza watalii wa ndani wachache walifika hifadhi ya Manyara lakini leo na kesho wanaimani wengi watajitokeza kushuhudia vuvutio katika hifadhi hiyo na pia kuona umuhimu wa uhifadhi kwa maslahi ya taifa.
WATANZANIA WACHACHE WAJITOKEZA KUTEMBELEA BURE HIFADHI ZA TAIFA WATANZANIA WACHACHE WAJITOKEZA KUTEMBELEA BURE HIFADHI ZA TAIFA Reviewed by KUSAGANEWS on June 03, 2017 Rating: 5

No comments: