MKAZI wa Kijiji cha Mesanga Mugumu
Wilayani Serengeti mkoani Mara, Wambura Muhonyi (32) amehukumiwa kunyongwa hadi
kufa baada ya kupatikana na hatia ya kushiriki katika mauaji ya Nyabaturi
Matoto akimtuhumu kuwa mchawi.
Mugumu anadaiwa akiwa na wenzake
wanne ambao wametoroka, walimuua Matoto ambaye ni mkazi wa kijiji hicho kwa
kumpiga kwa fimbo na kumkata kwa panga.
Akisomewa hukumu katika Mahakama Kuu
kanda ya Mwanza katika kesi ya mauaji namba 48/2014 na Jaji Rose Ebrahim alidai
kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa mwanasheria
wa Serikali, Venance Mayenga na kuungwa mkono na mashahidi wengine watatu wa
upande huo wa mashitaka akiwemo dada wa marehemu.
Awali katika kesi hiyo, mwanasheria
wa serikali Mayenga alidai kuwa Julai 16 mwaka 2010, majira ya mchana mtuhumiwa
Wambura katika kijiji cha Mesanga Mugumu Wilayani Serengeti, alishirikiana na
kikundi cha watu katika kijiji hicho wakiwemo watuhumiwa wenzake waliotoroka.
Watuhumiwa waliotoroka ni Mirumbe
Ngarita ,Gekene Wambura, Machota Tatwi na Marwa Mwita. Walikuwa wakimtuhumu
kuwa ni mshirikina na kwamba anamroga mke wa Wambura Wanchere kitendo ambacho
marehemu alikana.
Jaji Rose alisema “katika makosa ya
kuua kwa kukusudia chini ya kifungu cha sheria namba 196 ya makosa ya jinai
sura ya 16, kinaangalia nia ya kutenda kosa, mtuhumiwa alishiriki kwenda
nyumbani kwa marehemu kumchukua na kwenda kumsulubu hadi kifo chake kwa hali
hiyo nia ovu ilikuwepo, silaha zilizotumika”.
Alisema mtuhumiwa alionyesha
kudanganya mahakama kwa kudai hakuweka sahihi kitendo kilichodhihirishia
mahakama kuwa maelezo yake yalikuwa ya uongo ukilinganisha na ushahidi.
AHUKUMIWA KUNYONGWA KWA KUUA MCHAWI HUKO SERENGETI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment