Watu sita wameuawa na wengine 48 kujeruhiwa katika shambulio
linalodaiwa kuwa la kigaidi leo, jijini London, Uingereza
Polisi nchini humo wamesema, polisi walifanikiwa kuwaua
washambuliaji watatu kati yao
Ghasia zilianza baada ya gari moja kuingia ndani ya umati wa
watembea miguu, katika daraja kuu jijini London
Taarifa zimesema watu 20 waliojeruhiwa wamepelekwa katika
hospitali sita tofauti jijini London
Mwandishi wa BBC Holly Jones, aliyekuwepo katika eneo hilo
wakati wa shambulio hilo amesema gari lililohusika lilikuwa linaendeshwa na
mwanamume na lilikuwa linaenda kwa kasi
Alilipinda gari karibu nami na akagonga watu watano au sita
hivi. Aliwagonga wawili mbele yangu na kisha wengine watatu waliokuwa nyuma
yangu," Jones ameiambia BBC.
Sita wauawa katika shambulio la kigaidi London
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment