Mtoto
Doreen Mshana, manusura wa ajali ya Lucky Vincent, ameruhusiwa kutoka Hospitali
na sasa ameungana na wenzake wawili katika nyumba maalum wanamoishi, Marekani,
jimbo la Iowa.
Awali
wanafunzi wengine waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Mercy Hospital,
Sioux City, Saidia Awadh na Wilson Tarimo, waliruhusiwa kutoka
hospitali walimokuwa wakitibiwa.
Mbunge
wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, ameandika katika ukurasa wake wa
facebook na kueleza kuwa sasa Doreen, ameungana na wenzake baada ya hali yake
kuimarika.
Doreen,
alibaki hospitali hapo kutokana na majereha makubwa aliyopata na hivyo
kulazimika kufanyiwa upasuaji mkubwa wa uti wa mgongo.
Wanafunzi
hao walinusurika katika ajali ya basi la shule ya msingi ya Lucky Vincent,
iliyoua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva, Mei 6 mwaka huu, Karatu, Arusha.
Mtoto Doreen aruhusiwa kutoka hospitali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment