HATIMAYE ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU ANNA MGHWIRA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO
Rais Dk. John Magufuli jana amemteua
Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa
vyombo vya habari Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu,
Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo wa chama cha upinzani, anachukua nafasi
iliyoachwa wazi na Said Meck Sadiki.
Baada ya kukaa kimya kufuatia uteuzi
huo hatimayeLeo Jumapili June 4,2017 Kiongozi wa AICT Wazalendo Zitto Kabwe
ametoa ujumbe yafuatayo:
"Nimekuwa
naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea Taarifa za uteuzi kutoka
katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje ya nchi na kutokana na tofauti za
masaa bado hatujawasiliana nae. Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea
nchini.
Ninawataka
wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna masuala yanayohusu
maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.
Kabwe
Zuberi Ruyagwa Zitto,Mb
Kiongozi
wa Chama"
HATIMAYE ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU ANNA MGHWIRA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment