Mamia ya watu wamejitoza kutembelea Hifadhi ya Manyara na
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutokana na ofa ya kuingia bure hifadhini,
iliyotolewa na Serikali.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kutembelea hifadhi hizo wameipongeza
Serikali kwa ofa hiyo iliyowawezesha kushuhudia vivutio vya utalii
Cecilia Magandila, mkazi wa Mto wa Mbu wilayani Monduli,
amesema ameshuhudia vivutio vingi katika hifadhi ya Manyara ambavyo hakuwahi
kuviona.
Nimeona wanyama, chemchem za maji ya moto na mazingira
mazuri ambayo sikuwahi kuyaona,” amesema.
Mpishi mkuu wa hoteli ya Serena Manyara, Gervas Mhina na
wafanyakazi wenzake kwa nyakati tofauti wakiwa katika lango la kuingia Hifadhi
ya Ngorongoro na Serengeti wamesema uamuzi wa Serikali utasaidia kuwafanya
Watanzania kupenda uhifadhi.
Mhina amesema ni jambo la aibu kwa watalii kutoka Ulaya kuja
kutembelea hifadhi na Watanzania hata wanaoishi jirani, hawajawahi kuingia
hifadhini kushuhudia vivutio vya utalii.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Manyara, Dk Noelia Myonga amesema
kumekuwa na mwitikio mkubwa ambao kwa siku mbili zaidi ya Watanzania 300
wametembelea hifadhi hiyo.
Myonga amesema kujitokeza kwa watu hao kutasaidia kujua
umuhimu wa kutunza mazingira na kutembelea vivutio vya utalii.
Ofisa wa Idara ya Uhusiano ya Hifadhi ya Ngorongoro, Nickson
Nyange amesema zaidi ya watalii 400 wametembelea hifadhi hiyo kwa siku mbili na
hifadhi imeandaa waongoza watalii kusaidia wanaofika.
Nyange ametoa wito kwa Watanzania kutumia fursa ya ofa ya
bure kutembelea hifadhi za Taifa ili kuona umuhimu wa kutunza mazingira na
kujionea vivutio vya utalii.
Mamia wachangamkia ofa ya kuingia hifadhini bure
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment