Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRD), wamelaani
vikali kitendo cha kukamatwa kwa mratibu wa kitaifa wa mtandao huo Onesmo Ole
Ngurumwa.
Tamko hilo limetolewa leo Jumamosi na mwanasheria wa THRD,
Deogratius Bwire baada ya kukamatwa kwa mratibu huyo katika hoteli ya Blue Peal
saa tatu asubuhi wakiwa wanajiandaa kuingia kwenye uzinduzi wa kitabu cha
'sauti ya watetezi wa haki vyuoni
Bwire amesema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kukamatwa
kwao baada ya ya wakili Jones Semdodo aliyoko kituo cha polisi cha magomeni
kusema hakuna makosa yaliyoainishwa na wanasubiri maelezo kutoka juu.
Amesema Serikali na vyombo vya dola zifanye shughuli zao
kihalali pasi na kuonea watu ambao wanafanya shughuli zao kihalali.
Walia Ole Ngurumwa kukamatwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment