Makamu wa Rais, Samia Suluhu amewaagiza waajira wasiopeleka
au kuchelewesha michango ya wanachama kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii nchini
wachukuliwe hatua za kisheria ili kukomesha tabia hiyo
Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi jijini Mwanza wakati
anafungua semina ya maisha baada ya kustaafu,fursa ya mafao, uwekezaji
iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kwa ajili ya
wastaafu watarajiwa 450 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mwanza.
Amesisitiza kuwa waajiri wakichangia kwa mujibu wa sheria
kwenye mifuko hiyo watawezesha wanachama wao kupata mafao kikamilifu na kwa
wakati.
Kuhusu madeni ya Serikali kwa mifuko ya hifadhi ya jamii
nchini, Samia amewahakikishia wakurugenzi wa mifuko hiyo kuwa Serikali
inashughulikia madeni hayo na baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa
madeni basi malipo yatafanyika haraka iwezekanavyo.
Amesema kuwa Serikali itaendelea kuhakikisha michango ya
pensheni kwa wafanyakazi wa taasisi zinazopata ruzuku kutoka serikalini
inalipwa kwenye mifuko hiyo kwa wakati.
Samia awawashia moto waajiri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment