Serikali
itaendelea kuboresha huduma za afya kwenye vituo vya afya ,pamoja na Zahanati
mbalimbali katika jiji la Arusha.
Hayo
yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa arusha Bwana Mrisho Gambo katika
muendelezo wa ziara yake jijini Arusha
alipokuwa anazindua nyumba ya mtumishi iliyojengwa na serikali katika zahanati
ya NADOSOITO kata yaa Terati jijini hapa.
Nyumba hiyo
iliyogarimu kiasi cha shilingi milioni 66.7 ambapo ni mradi unatekelezwa kwa
awamu lengo ni kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika jiji la
Arusha kwa kuwaboreshea makazi watumishi waliopo pembezoni.
Pamoja na
hayo faida ya kukamilisha mradi huo umeongeza na kuboresha utoaji wa huduma za afya katika jiji la Arusha hasa
akina mama wajawazito na watoto kutoka kata za Muriet,Terati,Daraja mbili na
maeneo jirani.
Mradi huo wa
ujenzi wa nyumba ya mtumishi katika zahanati ya NADOSOITO ulianza june 15 mwaka
2016 na utakamilika 15 mwezi wa tano 2017 na mkandarasi anamalizia kwa kuweka
marumaru katika nyumba 2 na jiko.
""SERIKALI ITAENDELEA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA JIJI LA ARUSHA"" RC GAMBO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment