RC GAMBO ""WALIMU TUNAOMBA MUONGEZE JUHUDI KATIKA KUSAIDIA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU NAO WANAWEZA""

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametembelea na kujionea mradi wa darasa la watoto wenye ulemavu wa akili katika shule ya msingi Meru iliyopo Jijini hapa.

Akiwa katika shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 68miongoni mwao wasichana wakiwa 34 na wavulana 28 huku walimu viziwi wakiwa wawili na mtaalam mmoja wa kitengo cha I. C. T, Gambo alijionea mwenyewe jinsi wanafunzi hao wanavyofanya kazi kwa kutumia teknolojia hiyo.

Akisoma risala mbele ya Rc Gambo mwalimu Musa Lwambano alisema shule hiyo unajumla ya walimu 42 ambapo walimu 15 ni wa kitengo na 27 wa shule ya kawaida huku idadi ya wanafunzi ikiwa ni1,384 wavulana wakiwa ni 709 na wasichana wakiwa ni 675

Alisema shule hiyo inawafadhili kutoka nchi ya  Finland walioshirikiana na Halmashauri ya Jiji la Arusha lililotoa Sh, milioni 20 na wafadhili wakichangia zaidi ya sh, milioni 180  huku fedha hiyo ikisaidia kujenga jengo bora la ICT na kununua vifaa kama kompyuta mpakato (laptop) 184,deskitopu 5,Projekta 6,Sola 14,Scana Kamera 4,Ipad 22, Mashine ya Laminationi na printa 4.

Pia vijana viziwi wanne wamepata ajira katika kitengo hicho hukuwakimshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kwa kuwawezesha kupata maendeleo hayo shuleni hapo

Gambo alimpongeza walimu na wanafunzi wa shule hiyo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu na kuwasihi walimu kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wanafunzi hao ili waweze kupata ajira na kujikwamua kiuchumi

Awali Rc Gambo alijionea jinsi wanafunzi hao viziwi wakiimba wimbo wa Taifa kwa kutumia alama zao wakiongozwa na walimu wao ambao ni Veila Wilson na Neema Lema

Gambo anaendelea na ziara yake ya siku tano Jiji hapa kwa kuzindua miradi mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa barabara ya Mahakama na St, James uliogharimu Sh milioni 586. pamoja na kuzungumza na wananchi ili kutatua kero zao
RC GAMBO ""WALIMU TUNAOMBA MUONGEZE JUHUDI KATIKA KUSAIDIA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU NAO WANAWEZA"" RC GAMBO ""WALIMU TUNAOMBA MUONGEZE JUHUDI KATIKA KUSAIDIA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU NAO WANAWEZA"" Reviewed by KUSAGANEWS on April 27, 2017 Rating: 5

No comments: