Wananchi wa Kata ya
Muriet iliyopo eneo la Kwamrombo Jijini Arusha wataweza kunufaika na ujenzi wa
kituo cha Polisi ifikapo Juni mwaka huu mara baada ya kukamilika kwake.
Wananchi hao ambao
juzi walishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi uliofanywa na Mkuu Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo pamoja na wafadhili wa kampuni ya Lodhia Group ambao
wametoa Sh milioni 250 kwaajili ya ujenzi huo unatarajia kukamilika kati
ya Juni na Julai mwaka huu.
Wakitoa neno la
shukrani jana eneo la Morombo Jijini hapa wananchi hao ambao ni Rose Msai na
Sihaba Said walisema ujenzi huo utakapokamilika utawezesha wananchi
hao kupata huduma za usalama wa mali zao ikiwemo ulinzi kwani Kata
hiyo haina kituo cha Polisi na inategemea huduma za ulinzi na usalama kutoka
eneo la Mbauda ambapo ni mbali na eneo hilo.
Masai alisema ujenzi
wa kituo hicho utakapokamilika utawezesha wananchi wa Kata hiyo kupata huduma
za ulinzi na usalama kwani Kata hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali za
usalama kutokana na kukosekana kwa tukio hilo.
"Tunashukuru kwa
ujenzi wa kituo hiki cha polisi na pia tunashukuru kampuni ya Lodhia kwa
kutujengea kituo cha polisi ambacho kitahudumia sisi wananchi wa Kata hii kubwa
ambayo inachangamoto za kiuhalifu lakini uwepo wa kituo hiki utasaidia wananchi
kupata huduma mbalimbali "
Naye Mkurugenzi wa
Kampuni ya Lodhia Group, Arun Lodhia alisema kampuni yake imetenga faida ya Sh,
milioni 200 kwaajili ya wananchi ili kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili hivyo ujenzi wa kituo hicho cha Polisi utawezesha kuzuia
uhalifu.
Alisema ameamua
kujenga kituo hicho kwaajili ya kusaidia jamii ya wananchi wa Kata ya Muriet
kupata huduma bora za ulinzi na usalama ili kudhibiti matukio ya uhalifu na
watajenga nyumba kwaajili ya polisi wanatoa huduma kwa wananchi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo alisema kituo hicho kitasaidia wananchi kupata za ulinzi
na usalama ikiwemo ujenzi kwa kituo hicho ulioanza mwaka 2016
Wakati huo huo, Rc
Gambo amemwagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Arusha,
Mhandisi Gasper Msigwa kuhakikisha wanapeleka nguzo 800 za umeme kwenye maeneo
yote ya Kata ya Muriet pamoja na Terrat na wazisambaze kwenye maeneo hayo
kabla ya kupeleka kwingine
MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZINDUA KITUO CHA POLISI MURIETY
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 26, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment