Mkuu wa mkoa
wa arusha Bwana Mrisho Gambo amezindua mradi wa barabara yenye urefu wa
kilomita 0.65 katika kata ya kaloleni jijini arusha ambapo ni muendelezowa ziara
yake ya kikazi ya siku tano kwenye jiji la Arusha.
Akitoa
tarifa juu ya mradi huo injinia wa jiji Gaston Pascal kuhusu matengenezo ya barabara
ya st James Kaloleni iliyoinduliwa leo amesema
kuwa barabara hiyo imegaramiwa na mfuko wa barabara ambayo imetumia kiasi cha
ya shilingi milioni 586.5 mpaka kukamilika na inajumla ya mita 560.
Akizungumza
injinia Gaston amesema kuwa lengo la mradi huo ni maboresho ya ya miundombinu
ya barabara ndani ya kata ya kaloleni pamoja na wilaya ya Arusha kwa ujumla na
uamuzi wa kutengeneza barabara hiyo ulifikiwa kwa ajili ya kupunguza msongamano
wa magari katika jiji.
Baada ya
kupokea taarifa mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema kuwa kutokana na
utekelezaji mzuri wa mradi huo serikali itaendelea kuongeza fedha ili kuboresha
maendeleo hasa kwa upande wa miundombinu.
Hata hivyo
amesema serikali inaendelea kupeleka fedha katika halmashauri zote nchini
ikiwemo jiji la Arusha Arusha kwa
kiwango cha lami ambapo ni utekelezaji wa ahadi ya awamu ya tano ya Raisi Dokta
John Pombe Magufuli.
MKUU WA MKOA WA ARUSHA AZUNDUA BARABARA YA ST JAMES/KALOLENI ARUSHA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 26, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment