Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jiji la Arusha (AUWSA) Injinia Ruth Koya wamealazimika kunywa maji mbele ya wananchi wa Kata ya Olasiti wanayidai kuwa yanachumvi nyingi na hayafai kwa matumizi ya binadamu.
Gambo alilazimika kunywa maji hayo mara baada ya wananchi
kulalamika kuwa maji hayo ya Auwsa si salama kwa afya zao na yanachumvi kupita
kiasi hali inayosababisha usalama wa afya zao kuwa mashakani.
Wakitoa malalamiko yao Jijini hapa, mmoja kati ya wananchi
hao Hawa Ismail amesema maji yanatokana kwa nadra na eneo wanalochotea maji
hayo ni mbali hali inayopelekea baadhi yao kununua maji safi mjini au kwenye
magari maalum kama boza kwa kuchanhishana Sh, 70000 ili waweze kunywa maji
mazuri.
Ili kuonyesha kama maji haya ni salama ngoja ninywe mimi na
Mkuu mbele yenu halafu tuone kama tutapata madhara au la lakini niwahakikishie
kuwa maji haya hayana madhara yoyote kwa wananchi.
Awali Mkurugenzi wa Auwsa, Mhandisi Ruth Koya alisema maji
hayo hayanachumvi kubwa kama wanavyodai wananchi hao na yamepimwa na wataalam
wa maji ni salama kwa matumizi ya binadamu hivyo waendelee kuyatumia ili wakati
wakitafuta wataalam wa kuwasaidia kudhibiti chumvi hiyo.
Awali kabla ya Rc Gambo kuzindua ujenzi wa tenki la Maji
Mlima Burka Koya alisema mradi huo wa maji kutoka kisima cha
Magereza umesaidia uboreshaji wa maji katika Kata mbalimbali ikiwemo Kata
hiyo.
Amesema gharama za ujenzi wa tanki hilo ni Sh, milioni
135,020,960 hadi kukamilika kwake na utasaidia kutatua kero ya maji kwenye Kata
ya Muriet na Terrat ifikapo Julai mwaka huu
Gambo amesema kuwa yeye kama kiongozi mkuu wa serikali ya mkoa atahakikisha anawapa nguvu watumishi wa serikali ili kuendelea ili kuboresha huduma mbalimbali ambazo zimekuwa zikikabili wananchi wa hali ya chini.
Pia Rc Gambo alitoa rai kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,
Athumani Kihamia kutenga fedha kwaajili ya kulipa deni la walimu waliosimamia
mitihani wa darasa la nne kw shule za msingi badala ya kusubiri fedha kutoka
hazina na pindi zitakapokuja fedha hizo zitarejeshwa kwenye kifungu
kilichokopwa fedha hizo ili kuondoa manung'uniko ya walimu wanaodai malipo ya
mitihani pamoja na fedha za nauli.
Aidha Gambo amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athumani Kihamia kuhakikisha anatenga fedha za kuwalipa walimu waliosimamia mitihani wa darasa la nne mwaka jana ambao wanadai jumla ya Sh, milioni 52.
RC ANYWA MAJI MBELE YA WANANCHI KUWAHAKIKISHIA KWAMBA HAYANA MADHARA KIAFYA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 27, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment