Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia
Suluhu Hassan amewahimiza wananchi kudumisha na kuuenzi Muungano wa Taganyika
na Zanzibar na kuwahakikishia wananchi wa pande Mbili kuwa kero chache za
Muungano ambazo zimebaki zitamalizwa kwa mazungumzo kama hatua ya kudumisha
Muungano huo.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo kwa
nyakati tofauti katika Mahojiano na vyombo Mbalimbali vya habari katika
kuelekea katika Kilele cha Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
ambapo sherehe za kitaifa mwaka huu kwa mara ya Kwanza zitafanyika kwenye
Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma.
Makamu wa Rais amesisitiza kuwa tangu Muungano huo uasisiwe
umekuwa na manufaa makubwa kwa pande zote Mbili kwani jamii zimefahamiani na
kushirikiano vizuri katika shughuli za kiuchumi na za kimaendeleo hasa
uimarishaji wa ulinzi na usalama kwa wananchi wa pande Mbili.
Aidha,Amesema hatua zinazochukuliwa za kutatua kero za
Muungano kwa haraka ni jambo jema na la msingi kwani linalenga kuhakikisha
Muungano ambao umefikisha miaka 53 sasa unakuwa ni Muungano wa mfano wa kuigwa
Duniani.
Kuhusu elimu ya Muungano wa Vijana, Makamu wa Rais Mhe Samia
Suluhu Hassan amesema upo umuhimu mkubwa kwa taasisi za Kiserikali za pande
Mbili kuweka mikakati mizuri ya kuelemisha vijana wa sasa kujua umuhimu wa
Muungano ili waweze kuuelewa na kuudumisha.
Amesema kwa sasa vijana wengi wanafuatilia sana mitandao ya
kijamii hivyo ni muhimu kwa taasisi za kiserikali zinazoshughulia Muungano
kuweka utaratibu wa kupeleka ujumbe mbalimbali kuhusu Muungano kwa jamii hasa
vijana kwa ajili ya kuwaelimisha faida za Muungano.
Makamu wa Rais pia amehimiza makundi mbalimbali ya kijamii
wakiwemo viongozi wastaafu nchini waendelee na jitihada zao katika kuelimisha
umma ili kuuelewa vizuri Muungano kwa ajili ya faida ya jamii nzima na ya Taifa
kwa ujumla.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
DODOMA.
25-April-2017
Samia Suluhu: Kero za Muungano zitatatuliwa kwa mazunguzo ya pande Mbili
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment