Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi, The
Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na kusema chama cha CUF
hakina walinzi wa chama wenye bastola wala hakina walinzi wanaozunguka mitaani
kufanya doria.
Julius Mtatiro ametoa ufafanuzi huo
leo baada ya Mkurugenzi wa Habari CUF Taifa, ambaye anamuunga mkono Profes
Ibrahim Lipumba ndugu Abdul Kambaya kukiri kuwa ni kweli wao walituma
vijana kwenda kwenye Kata ya Mabibo kufanya doria.
"Siku ambapo kikao kinafanyika
Vinna Hotel, vijana wetu pia walikuwa kwenye doria, tulipozungumza na vyombo
vya habari tulikiri na tunaendelea kukiri hatuna sababu ya kukataa kwamba
tulituma vijana wetu na walikwenda kwenye doria" alisema Kambaya
Kufuatia taarifa hiyo ya Kambaya Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi, The Civic United Front (CUF) Julius Mtatiro amefunguka na
kusema wao kama CUF hawana walinzi wa chama wenye bastola hivyo amelitaka jeshi
la polisi limtumie huyu Kambaya kueleza kijana aliyekuwa na bastola yuko wapi
na walikodishwa kutoka wapi.
"Leo amekiri kuwa lile Zombi
lililopigwa na wananchi, Mabibo, eti lilitumwa na genge la Mungiki/Lipumba ili
kufanya doria kwenye kata ya Mabibo. Yani eti Lipumba ana jeshi lake
linalofanya doria na kupiga watu mitaani. Sasa Polisi wasitafute mchawi, huyu
Abdul Kambaya aeleze lile zombi lililokuwa na bastola liko wapi na waliikodisha
kutoka wapi? Alihoji Mtatiro
Mbali na hilo Mtatiro alizidi
kusisitiza kuwa wao hawana walinzi wa chama
"Halafu, eti huyo msemaji wa
Lipumba anasema "Zombi" hilo lililokamatwa ni "mlinzi wa
chama". Napenda ifahamike kuwa CUF haina walinzi wa chama wenye bastola,
na pia hakuna chama cha siasa chenye walinzi wanaozunguka mitaani kufanya
doria, wameajiriwa na serikali ipi? Alihoji Mtatiro
Mtatiro: CUF haina walinzi wa chama wenye bastola
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 25, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment