Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima
amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha
dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).
Amesema kuwa treni hiyo itatumika siku za ibada kubeba
waumini huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu. Lakini pia alisema atakuwa
tayari kuruhusu itumike kubeba abiria wa kawaida.
Askofu Gwajima aliyasema hayo jana kanisani kwake, ambapo
alieleza gharama za treni hiyo ni TZS bilioni 11 lakini hakusema ni lini hasa
atainunua.
“Siku moja nilimchukua mwalimu Bihagaze, alikuwa mwalimu
wangu wa Biblia, nikamwambia twende nikakuonyeshe mji wa mwanakondoo,
nikamchukua na helkopta hadi shambani ambapo ni mji utakuwa na mahoteli,
universities, kituo cha mafuta na kila kitu,” alisema.
Alifafanua kuwa katika mji huo, kuna ramani inaonyesha kuwa
reli inapita katikati. “Alipopaona akasema mbona kuna reli inapita katikati,
nikamwambia nitanunua treni, akashangaa akaniuliza, treni ni shilingi ngapi?
Nikamwambia dola milioni nne na mabehewa yake dola milioni tano hivi, akasema
nikulipie? Nikamwambia nitanunua mwenyewe. Akapiga magoti kusujudu nikamwambia
yapo mengi yanakuja,” alisema Askofu Gwajima huku waumini wake
wakimshangilia kwa shangwe.
Ujenzi wa reli uliozinduliwa na Rais Dkt Magufuli Aprili 12
mwaka huu, utakamilika ndani ya miezi 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanzia
Dar es Salaam hadi Morogoro, treni ikiwa na uwezo wa kukimbia umbali wa
160km/hr. Treni itakuwa na jumla ya mabehewa 100.
Askofu Gwajima Kununua Treni ya Umeme
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2017
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 24, 2017
Rating:


No comments:
Post a Comment