MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AAGIZA KURUDISHWA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA JUMA IDI KUJA KUJIBU TUHUMA ZINAZOMKABILI



Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo amemuagiza katibu tawala mkoa Richard Kuitega kuandika barua Kwenda Tamisemi ya Kuwasimamishwa kazi watumishi watatu wa halmashauri akiwemo aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la Arusha Bwana Juma Iddi.

Akizungumza katika mkutano wa watumishi,wazee,vikundi vya akina wanawake, vijana, madiwani,watendaji wa kata ,viongozi wa dini na wakimila,katika ziara yake ya siku tano aliyoianza mkoani Hapa kwa ajili ya kuzungumza na wazee,kuzindua miradi,pamoja na kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo.

Gambo amesema kuwa watumishi hao ni Bakari  Salum Aliyekuwa Mganga wa Jiji la Arusha ,aliyekuwa mweka Hazina Kessy na Mkurugenzi Juma Idd kwa kukiuka sheria ya manunuzi ya umma.

Moja kati ya tuhuma hizo ni matumizi ya fedha ya posho ya ukaguzi  kwa shilingi milioni 64.7,ambazo walijilipa watumishi watumishi zaidi ya 2O.

Aidha gambo amewataja watumishi hao kuwa ni Allen Sumari,Amani lyimo,Anjela mhetu,babila Shilogela,Baraka Ahmad,Cloudia Kkidunda,Cleti Sadala,Dickson Laizer,Dkt.Bakari Salum,Dikson lazier,dkt,Baraka Munde,dkt,Yunus Minja,dkt,Isri Ismail,dkt.Japhet Kiuvuyo,Dkt.Josiah Mlay,dkt,Thomas Kway,Dkt.Elly Mrema,Farida Minja,fausta kambaga,Goodluck Ekwabi,hamida kaligaliga,happy saigurani,Hassan abdallah ,james lobikoki,Jane Baralukuliliza, na Joel Msuya.

Amesema huko nyuma kumekuwa na utaratibu wa kutumia fedha za umma kama shamba la bibi na kunufaisha watu wachcahe na sio kunufaisha wananchi wengi hivyo watakaobanika kukiuka taratibu basi na kuvunja sheria hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AAGIZA KURUDISHWA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA JUMA IDI KUJA KUJIBU TUHUMA ZINAZOMKABILI MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AAGIZA KURUDISHWA  ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA JUMA IDI KUJA KUJIBU TUHUMA ZINAZOMKABILI Reviewed by KUSAGANEWS on April 25, 2017 Rating: 5

No comments: