Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete ameipongeza sekta ya ujenzi kwa kuondoa aibu kwa watanzania kulazimika kupita nchi jirani wakati wa kusafiri kutoka mkoa moja kwenda mwingine ndani ya nchi huku akiweka wazi kuwa akistaafu maskani yake yatakuwa kijijini Msoga,Bagamoyo mkoani Pwani.
Rais Kikwete ameyasema hayo katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini
Dar es Salaam katika hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na taasisi pamoja na
idara zilizopo chini ya wizara ya ujenzi na kuongeza kuwa serikali yake
iliweka kipaumbele katika sekta ya ujenzi kwa makusudi kwa kuwa
usafirishaji ndio nguzo kuu ya kukuza uchumi huku akiipongeza wizara ya
ujenzi kwa kuliondolea taifa aibu ambapo watanzania walilazimika kupita
nchi jirani wakiwa safarini kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine kutokana
na ubovu wa barabara.
Aidha rais Kikwete mbali ya kuelezea namna sekta ya ujenzi
inavyochangia kukuza uchumi wa nchi na kuondoa umasikini hakusita
kummwagia sifa kem kem waziri wa ujenzi Dr.John Pombe Magufuli huku
akimuelezea kuwa ni mchapa kazi makini asiyeyumbishwa na rushwa na
kwamba moja ya wizara ambazo hazikumnyima usingizi wizara ya ujenzi ni
miongoni mwao.
Waziri wa ujenzi Dr.John Pombe Magufuli kwa upande wake ameelezea
namna Tanzania ilivyopiga hatua kubwa za kimaendeleo kwa kujenga miundo
mbinu ya barabara ambapo zaidi ya kilomita 17 elfu zimejengwa kwa
kiwango cha lami kwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha zake za ndani
lakini pia namna sekta ya ujenzi ilivyosaidia kukuza uchumi wa nchi.
Chanzo Itv
Rais Kikwete ameipongeza sekta ya Ujenzi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment