Jeshi la polisi limetakiwa kubadilisha mbinu za upelelezi wa makosa ili kuendana na Sayansi na Teknolojia.
Waziri
wa maendeleo ya Sayansi na Tekonolojia nchni Profesa Makame Mbara
amelitaka jeshi la polisi nchini kubadirisha mbinu za upelelezi wa
makosa ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia
yanayobadirika kila wakati ili kujenga uwezo kwa kuwalinda wananchi na
taifa kwa ujumla.
Akifungua mafunzo ya sheria ya makosa ya mtandao inayoanza kutumika
rasmi Septemba mosi mwaka huu kwa makamishna makamanda wa jeshi la
polisi, Profesa Mbarawa amesema jeshi la polisi linadhamana ya kusimamia
sheria hiyo hivyo linapaswa kuielewa zaidi ili kuweza kuwabana watenda
makosa ya kimtandao katika vyombo ya utoaji haki ikiwemo mahakama.
Wakizingumzia sheria hiyo, mwakilishi wa mkuu wa jeshi la polisi
nchni kamishna Mussa Ali Mussa amesema makosa mengi yanayotendeka siku
hizi ikiwemo matusi, kashfa yanatendeka kwa njia ya mitandao ya
mawasiliano hivyo kupitishwa kwa sheria hiyo pamoja na kujengewa uwezo
kutalipa nguvu jeshi la polisi kufanya kazi kwa ufanisi.
Jeshi la polisi limetakiwa kubadilisha mbinu za upelelezi wa makosa ili kuendana na Sayansi na Teknolojia.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment