Chama cha mapinduzi CCM kupitia wenyeviti wa mikoa wa chama hicho,
wameapa kukipigania chama hicho hadi hatua ya mwisho na kuwa hakuna
chama mbadala cha kutatua matatizo ya wananchi zaidi ya CCM kwa kuwa
vyama vingi vya kisiasa hapa nchini viko kwa ajili ya maslahi ya
viongozi huku wananchi wakitakiwa kutafakari na kuwachambua wagombea ili
kufahamu azma yao ya kusaka madaraka na kutofautisha wale wenye maslahi
binafsi na wale wenye nia ya kuleta maendeleo nchini.
Mwenyekiti wa wenyeviti wa chama hicho Bwana Ramadhani Madabida
ameyasema hayo mkoani Dodoma mara baada ya kumalizika kikao cha
halmashauri kuu cha kupitia majina ya wagombea udiwani na ubunge na
kuongeza kuwa kwa tathmini ya haraka wanaoondoka CCM kwa sasa ni wale
walioshindwa kupata nafasi ndani ya chama hicho au majina yao kukatwa na
vikao halali ndani ya chama hicho kikongwe nchini.
Awali mgombea wa nafasi ya urasi wa jamuhuri ya mungano wa Tanzania
kupitia chama cha mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Joseph Magufuli,
amewaomba wenyeviti hao wa CCM wa mikoa nchini kuwa wamoja katika
kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais wabunge na
udiwani.
Katibu mkuu wa chama hicho komredi Abdulrahman kinana amewaeleza
wenyeviti hao juu ya chama hicho kujipanga vizuri kwenye uchaguzi huu
kwa kutumia njia ya anga, majini na nchi kavu kwa kuwa na ilani bora
inayokidhi matakwa ya wananchi walio wengi, kuweka mgombea anayekubalika
na wananchi, huku akiwasisitizia wenyeviti hao kuwa chama hicho,
kimeaminika na watanzania wengi kwa mtu mmojammoja ama vikundi,hatua
itakayopelekea chama hicho kuibuka na ushindi wa kishindo chini ya
uratibu wa katibu mkuu mwenye uzoefu ndani ya chama cha mapinduzi.
Dkt Magufuli apewa msimamo na wenyeviti wa CCM mikoani.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 16, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment