Kwa nini taasisi za
kijamii zisipendekeze awamu moja ya uongozi wa Serikali iwe na miaka sita au
saba badala ya kuhimiza utawala wa awamu mbili za miaka mitano mitano? Nadhani
wafanyie kazi jambo hili.
Barani Afrika,kitendo cha
kiongozi wa Serikali (Rais) kubadilisha katiba ili akae madarakani kwa awamu ya
tatu kimekuwa kikilalamikiwa na taasisi za kijamii na Jumuiya za Kimataifa.
Hivi karibuni rais wa
Burundi, Pierre Nkurunziza alibadilisha katiba ya nchi hiyo kwa ajili ya
kuwania urais kwa awamu ya tatu, pia rais wa Rwanda, Paul Kagame ameanzisha
mjadala nchini kwake wananchi waamue kama wanakubali awanie urais kwa awamu ya
tatu.
Wananchi wa Nigeria,
Malawi, Zambia, Tanzania na Burkina Faso wenyewe wamekataa suala la awamu tatu,
lakini haijawasaidia, kwani bado zina matatizo ya kiuchumi, kijamii na matatizo
ya kisiasa kama rushwa.
Matatizo hayo yanatokana
na udhaifu wa wizara za Serikali, hakuna wizara imara. Hata hapa nchini hakuna
wizara imara, ndiyo maana wizara inayosimamia michezo siyo imara. Kwa hiyo
sidhani kama ni kweli suala la awamu tatu linazuia maendeleo ya nchi, kwani
kiongozi kama anaweza kujenga wizara zake imara ni anaweza tu na kama hawezi
basi hawezi tu hata ukimpa awamu nne.
Unajua nimeenda nchi
nyingi za Afrika na nilichokiona barani Afrika ni kwamba tunaiga demokrasia za
nchi za Ulaya bila kuelewa maana ya demokrasia. Viongozi wengi wa Afrika
wanataka awamu ya tatu kwa sababu wanajua kwamba baadhi ya nchi za Ulaya kuna
viongozi (Mawaziri Wakuu na Machansela) wameongoza kwa awamu tatu. Hata hivyo
viongozi hao wa Afrika wanaweka kando hoja ya msingi kwamba nchi hizo za Ulaya
zinatumia mfumo wa uongozi wa kibunge (Chama ambacho kinashinda viti vingi vya
ubunge ndiyo kinatoa Waziri Mkuu anayeongoza Serikali na hakuna rais, lakini
nchi za Afrika hazina mfumo huo zina mfumo wa kuwa na rais anayeongoza Serikali
na nchi).
Katika mfumo huo wa
kibunge wa nchi hizo za Ulaya, viongozi wa taasisi na Waziri Mkuu wanaweza
kuondolewa madarakani kiraisi sana kama wapiga kura au wanachama wao
wamewachoka.
Tunatakiwa tukumbuke
kwamba nchi za Ulaya zina viwanda vingi, wananchi wana elimu ya juu ya uraia na
wapiga kura hawanunuliki. Ni kinyume kabisa na nchi za Afrika ambazo viongozi
wanataka kuongoza kwa awamu tatu huku wakishindwa kujenga wizara ambazo ni
imara moja ya wizara hizo ikiwa ile inayosimamia michezo.
Sasa unaweza kujiuliza,
je, kiongozi kuongoza kwa awamu tatu ni kitendo cha kuzuia maendeleo? kwa
upande wangu naona siyo kweli. Kiongozi kuongoza kwa awamu tatu siyo kosa kama
wizara zitakuwa huru, imara na zinazofanya kazi kwa ufanisi, rushwa itakuwa kwa
kiwango cha chini, chaguzi zinaendeshwa kwa uhuru na haki, wapiga kura
watakataa kununuliwa na wanasiasa watakuwa siyo wala rushwa.
Ninasema hivyo kwa
sababu, kama mtakumbuka rais wa kwanza wa Namibia, Sam Nujoma baada ya
kusimamia vizuri nchi yake na kujenga wizara zake imara ndani ya awamu mbili
alipewa awamu ya tatu na wananchi wa nchi hiyo bila ya kubadilisha katiba, kwa
hiyo tatizo siyo awamu tatu ila ni kuwa na wizara imara.
Ndiyo, hata mimi
ninaamini kinachotakiwa ni wizara imara ikiwamo wizara ya michezo. Kwa sababu
hatuna wizara imara nchini, ndiyo maabu haitengewi fedha za miradi ya
maendeleo, pia hata wizara nyingine nazo hazifanyi vizuri tazameni muone.ana
sishangai kuona hakuna maendeleo ya michezo kwani wizara inayoongoza michezo ni
kama haipo kwa sasa
mwananchi
MTAZAMO : Wizara ya michezo ni kama haipo, tazameni vizuri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment