Dar es Salaam. Mwimbaji aliyetamba na video ya “Ole Themba”, Linah Sanga
amesema kuwa ili kuwa msanii wa kimataifa kuna gharama kubwa tofauti na wengi
wanavyodhani.
Linah alisema anafikiria
kila siku kuendelea kufanya kazi nzuri za kimataifa kama viedo ya ya Ole
Themba, lakini kila anapofikiria kwenda tena Afrika Kusini kurekodi anakumbuka
namna alivyotumia pesa nyingi kukamilisha wimbo huo.
“Siyo kwamba sipendi
kurudi tena Afrika Kusini kwa ajili ya kufanya video nyingine, bali kufanya
kazi hizo nje ya kunahitaji pesa nyingi kuliko hapa Bongo,” alisema Linah.
Linah alisema kufanya
video au audio katika nchi zilizoendelea kuna gharama kubwa, lakini ni lazima
msanii atumie muda mwingi kwa ajili ya kukaa hotelini, gharama za usafiri
pamoja na malipo makubwa ya kazi.
“Ninapenda kufanya kazi
tofauti zenye kiwango cha juu na hivi ndivyo ilivyo kwa wasanii wengi, lakini
matumizi makubwa ya fedha kwa kazi za kimataifa ni makubwa kinyume na watu
wanavyodhani. Ingawa kazi inakuwa nzuri, lakini gharama zake usipime, pengine
waandaaji wetu wa Bongo wanapaswa kujifunza zaidi kutoka kwa wenzao ili
kupunguza wimbi la gharama za kwenda kufanya video huko,” alisema Linah.
Chanzo: Mwananchi
Linah akumbuka Dola 47,000 za Ole Themba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment