TASNIA
ya filamu imezidi kukua na kusonga mbele kila siku, thamani ya wasanii
wanalipwa fedha nyingi kwa kushiriki filamu moja jambo linalomfanya
mtayarishaji kutumia wasanii wachache kwa filamu yake lake katika sinema ya
WAKE UP imevunja rekodi kuwashirikisha nyota wengi.
Akiongea
na waandishi wa Habari mtayarishaji wa filamu hiyo Manaiki Sanga amesema kuwa
sinema hiyo ilikuwa na kazi kubwa kwani hata kama mwigizaji angetaka kuigiza
bure shughuli ilikuwa kuwahudumia mahitaji yao kwani ni mastaa wenye mahitaji
makubwa katika maisha yao.
“Nashukru Mungu kwa
kuniwezesha kufikia ndoto zangu kila siku nilikuwa natamani kufanya kitu cha
kipekee katika tasnia ya filamu na nimeweza kuwashirikisha wasanii nyota wote
,”“Nimetumia fedha nyingi sana lakini lengo ni kuwa tofauti na wenzangu katika
utayarishaji ilikuwa ni kazi ngumu katika kuwapata na kuwashirikisha, namshukru
sana Lamata Director wangu,”
anasema
Manaiki.
Filamu
hiyo ambayo ipo tayari inatarajia kutoka mwezi wa nane mwaka huu
imewashirikisha wasanii kama Kajala Masanja, Amri Athuman ‘King Majuto’, Hemed
Suleiman, Irene Uwoya, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Tausi Mdegela, Yusuf Mlela,
Manaiki Sanga, Chuchu Hans, Mutrah, Asha Boko na nyota wanaofanya vizuri katika
filamu Bongo Movie.
Sinema
hiyo ambayo inaleta mapinduzi katika tasnia ya filamu Bongo itasambazwa na
kampuni ya usambazaji wa filamu za kibongo ya Steps Entertainment nchi nzima na
kuona jinsi wasanii walivyoshindana humo na kuinogesha filamu hiyo
FILAMU YA KWANZA TANZANIA KUCHEZWA NA NYOTA WENGI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment