Dar/Mikoani. Katika kile kinachoonekana kuendelea kujiimarisha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimegawana maeneo mbalimbali nchini vikifanya mikutano ya hadhara na mafunzo kwa viongozi wake ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa ushindi.
Ukawa unaundwa na vyama vya Chadema, NLD, NCCR-Mageuzi na CUF.
Chadema kilianza ziara zake mikoani wiki zilizopita baada ya kuzindua mkakati wake uitwao ‘Hakuna kulala, Hakuna kula, Mpaka Kieleweke’ nchi nzima wakati timu ya NCCR-Mageuzi ikiweka kambi mkoani Kigoma kwa kile ilichokiita kuimarisha majimbo ya kimkakati.
Sanjari na vyama hivyo, CUF tangu juzi kiliingia katika moja ya ngome zake, mkoani Mtwara pamoja na mipango mengine ya kiushindi, kinahamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha kupiga kura.
Jitihada za Ukawa kuzunguka mikoani zinakuja ikiwa ni majuma kadhaa tangu Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiongozwa na Katibu Mkuu wake Abdulrahman Kinana kilipomaliza ziara ya kujiimarisha na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.
Pia, ziara hizo ziligongana na zile za Chama cha ACT - Wazalendo zilizosababisha Chadema na chama hicho kipya kugongana Butiama.
ACT - Wazalendo kinachoongozwa na Zitto Kabwe kilihitimisha ziara yake ya kimkakati katika mikoa tisa inayoonekana kuwa ngome ya CCM, wiki iliyopita wilayani Bariadi, Shinyanga na kuvuna wanachama zaidi 6,000 katika mikoa hiyo.
NCCR-Mageuzi ipo Kigoma
Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Mosena Nyambabe alisema jana kuwa Ukawa ina mikakati inayofanana ndani ya vyama vyao ya kuhakikisha inajiimarisha kisiasa nchi nzima ili ishinde Uchaguzi Mkuu.
Alisema siku 10 zilizopita, timu ya NCCR ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti - Zanzibar, Haji Hamis Hamad ilianza ziara Kigoma kuhakikisha majimbo ya mkoa huo yanaendelea kuwa ngome yake.
“Kigoma nzima ina majimbo yetu ya kimkakati na Ukawa wameshatukabidhi sasa kilichobaki ni kufanya ‘political management’ (usimamizi wa kisiasa) katika kiwango kinachotakiwa.
“Katika kikosi hicho, pia wamo Katibu Mwenezi, David Kafulila, Katibu Mkuu Mstaafu, Samuel Ruhuza na Kamishna wa Kagera, Peterson Mshenyela na wengineo,” alisema Nyambabe.
Chanzo; MWANANCHI

Ukawa waanza kugawana nchi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment