Ni kesi iliodumu takribani
miaka saba na kuziteka hisia za wananchi wengi wa Tanzania kwani ilikuwa
ikiwahusisha viongozi wa ngazi za juu serikalini kwa kashfa ya kutoa msamaha wa
kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza bila kufuata kanuni.
Mawaziri hao wamepelekwa katika
gereza la Keko jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa waziri wa fedha Bazil
Mramba akatiwa hatiani katika mashitaka yote 11 yaliyokuwa yakimkabili ambapo
mashitaka 10 yalikuwa ni ya matumizi mabaya ya madaraka na shitaka la 11 likiwa
ni kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11. 7 sawa na takribani
dola elfu tano za Marekani.
Daniel Yona aliyepata kuwa Waziri
wa nishati na Madini, naye akitiwa hatiani kwa makosa matano ya matumizi mabaya
ya madaraka na kuisababishia hasara serikali.
Mshitakiwa mwingine wa tatu
ambaye alikuwa katibu Mkuu wa zamani wa wizara ya fedha ya Tanzania, Aggrey
Mgonja aliachiwa huru baada ya upande wa mashitaka kushindwa kuthibitisha
mashtaka yote 11 yaliyokuwa yakimkabili
Kifungo kwa mawaziri wa zamani Tanzania
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment