Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene amekea tabia ya watu kukusanyana na kuvamia watu walioko kwenye faragha kwa kisingizio cha fumanizi akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na utu na watakamatwa wakigundilika.
Simbachawene ametoa
kauli hiyo leo Ijumaa Agosti 6,2021 ambapo amesema baadhi ya watu wamejingea
mazoea ya kuwavamia watu wenye uhusiano ya kimapenzi wakiwa kwenye faragha zao
mahali wanapokuwa katika nyumba au hotelini.
“Tabia hii imeshamiri
sasa kama ambavyo video nyingi zinarushwa rushwa mitandaoni, leo nitumie fursa
hii kutoa msingi wa kisheria lakini kukemea tabia hii ambayo imeanza kuonekana
inaota mizizi. Ni kinyume cha sheria kabisa kuwaingilia watu walio kwenye
faragha,” alisema
“Wakati mwingine watu
wanafanya hivyo kwa kisingizo kuwa wamefumania, hakuna fumanizi ambalo linaweza
kupangwa na kikundi cha watu, wanawake na wanaume wanapanga kwenda kuwavamia na
kuwaingilia uhuru wao waliopo faraghani, kitendo hicho ni kinyume cha sheria ,”
Amesema hata kama ni
fumanizi litakuwa pale ambapo si jambo la kupangwa na huyo anayefumania awe na
ndoa halali na cheti halali cha ndoa lakini sio kwa mtu ambaye ulikuwa naye tu
“Huwezi kusema umemfumania hawala yako, mahusiano ya hawala ni ya kupita”.
Amesema tabia hiyo
inakiuka misingi ya utawala bora, heshima na utu na hasa heshima ya wanawake
kwakuwa wanaodhalilishwa sana katika hilo ni kina mama ambao walishakuwa na
uhusiano na mwanaume fulani wakaachana akawa na mwingine halafu yule wa mwanzo
anamfumania.
“Suala la kudhalilisha watu wako uchi wa
mnyama na wanapata kipigo hilo haliwezi kukubalika katika nchi yetu, kwa nafasi
yangu nachukua nafasi hii kuliagiza jeshi la polisi wahakikishe wanafuatilia
matukio haya hususani hili linalozunguka kuanzia jana, wahakikishe wale wote
waliohusika wanakamatwa,” amesema Simbachawene.
No comments:
Post a Comment