KESI ya Unyang'anyi wa
kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya
na wenzake wawili imeshindwa kuendelea baada ya Sabaya kuugua na kushindwa
kugoka mahakamani.
Mkaguzi Msaidizi wa
Magereza, Ramadhani Misanga leo ameieleza mahakama ya hakimu mkazi
Arusha, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo kuwa Sabaya anaumwa na
amepatiwa dawa na ametakiwa kupumzika kwa siku moja.
Mkaguzi msaidizi wa magereza, Inspekta Msaidizi, Ramadhani Misanga nashukuru
mheshimiwa hakimu mteja wetu na wa mawakili wa utetezi hajaweza kugika
kwa sababu kama ilivyo kawaida mahabusu wote baada ya kupata kifungua kinywa
wale ambao hawajisilii vizuri huenda kumuona daktari.
Misanga alisema kuwa
asubuhi alipata taarifa kutoka kwa mkuu wa gereza kuwa mshitakiwa wa kwanza (
Sabaya) hajisikii vizuri amepewa dawa na mapumziko ya siku moja.
"Nikiwa ofisini
mshitakiwa wa kwanza alinifuata kunijuza hajisikii vizuri ameenda kwa daktari
amepewa dawa na ana mapumziko ya siku moja hivyo kesho atahudhuria
mahakamani lakini kwa kuwa ni ugonjwa si hakika sana kama atakuwa amepona na
aweze kufika," Misanga aliieleza mahakama .
Awali Wakili wa
Serikali Mkuu, Tumaini Kweka, aliieleza mahakama hiyo kuwa shauri limekuja
mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa saba, Mkuu w upelelezi wilayani Arusha,
Gwakisa Minga kuendelea na ushahidi wake pale alipoishia jana.
" Mheshimiwa
hakimu tumepata mawasiliano kutoka uongozi wa magereza ambao unawaleta hawa
washitakiwa kuwa mshitakiwa namba moja, Lengai ole Sabaya ameshindwa kufika
mahakamani kwa sababu za kiafya," wakili huyo wa serikali ameieleza
mahakama.
Ameendelea kueleza
mahakamani hapo kuwa kwa mujibu wa sheria ya usikilizaji wa mashauri ya jinai kifungu
cha 196 na sheria inayosimamia mwenendo wa mashahuri ya jinai sura ya 20 kama
kilivyofanyiwa wanasema juzuu ya mwaka 2019 inasema usikilizaji wa shauri
la jinai ni lazima ufanyike mshitakiwa akiwa mahakamani.
Hata hivyo Wakili
Kweka aliieleza mahakama hiyo kuwa shauri linaweza kuendelea bila mshitakiwa
kuwepo mahakamani kwa sababu mbili tu.
" Mheshimiwa
hakimu kifungu 197 cha sheria inayosimamia uendeshaji wa mashauri ya
jinai kinaeleza mazingira gani mahakama inaweza kuendelea bila mshitakiwa
kuwepo mahakamani," ameeleza wakili Kweka na kuongeza
.Kutokana na habit
ya mshitakiwa mahakama itaagiza shauri liendelea bila mshitakiwa kuwepo. Mbili
endapo mshitakiwa hatakuwa mahakamani kwa matatizo ya kiafya na anawakilishwa
na mawakili na ameridhia kwa mawakili wake kuwa kesi iendelee pasipo uwepo
wake....
..Hili letu liko
kwenye kifungu cha pili lakini hatujui mawakili wake kama wamepewa ridhaa
na mshitakiwa tuendelee. Sisi tuko tayari kuendelea na shahidi wetu.
Ni hayo tu,".
Baada ya maelezo hayo
wakili wa mshitakiwa wa kwanza, Dancan Oola aliieleza mahakama hiyo kuwa
anakubaliana vifungu vyote vya sheria alivyosoma wakili viko sawa.
"Swali kama
tumepewa ridhaa ya kuendelea, hatujapewa hiyo ridhaa hivyo mheshimiwa tunaomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kusikilizwa kwa ushahidi,". wakili Oola aliieleza
mahakama.
Baada ya wakili mkuu
wa serikali, Kweka na Wakiki wa utetezi kueleza hayo Hakimu Mkazi Mwandamizi,
Amworo aliwataka afisa wa magereza kutoa uelewa juu ya hali ya mshitakiwa
ndipo Mkaguzi Msaidizi wa Magereza, Misanga akatoa maelezo.
Baada ya maelezo hayo
hakimu ameahirisha shauri hilo mpaka kesho Agosti 5, mwaka huu shauri hilo
litakapokuja mahakamani hapo kwa ajili ya shahidi wa saba kuendelea na ushahidi
wake.
Washitakiwa wengine
Silvester Nyegu na Daniel Mbura walirejeshwa mahabusu kwenye gereza la
Kisongo kwani kesi inayowakabili haina dhamana.
No comments:
Post a Comment