NENO LA MWISHO LA ALIYEUAWA KWA RISASI SINZA

 
Mdogo wa Marehemu  (Gift Mushi) analiyeuawa kwa kupigwa risasi Sinza Dar es Salaam, Edga Kombe ameleezea neno la mwisho la kaka yake  kabla ya umauti kumfika.

Kombe ambaye ni mdogo wa marehemu upande wa baba mdogo amesema marehemu kabla ya umauti alisema “nitakuzika na wewe unizike”.

Akizungumza  Kombe amesema “nitamzika ndugu yangu kwa sababu alisema nimzike na nitatimiza ahadi yetu, hii yenyewe ni cheni yake nilimvua mochwari tulivyokuwa tunamsafisha.”

Tukio la mauaji  lilitokea jana  Julai 17, majira ya saa kumi na moja jioni likimuhusisha kijana Alex Korosso alimaarufu Simba ambaye alimpia risasi sita maeneo tofauti ya mwili wa Gift Mushi kisha kujiua kwa kujipiga risasi.

NENO LA MWISHO LA ALIYEUAWA KWA RISASI SINZA NENO LA MWISHO LA ALIYEUAWA KWA RISASI SINZA Reviewed by KUSAGANEWS on July 18, 2021 Rating: 5

No comments: