Ombi hilo
liliombwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyemuandikia barua Rais
Samia mapema Aprili mwaka huu akiomba kuonana na uongozi wa chama hicho kwa
ajili ya kumueleza masuala mbalimbali.
Mnyika ameeleza hayo leo Jumapili Aprili 25, 2021 kupitia akaunti yake ya
Twitter akiandika kuwa “Naomba kuwapa taarifa rasmi kuwa Aprili 20, 2012 tulipokea
majibu ya barua ya Mwenyekiti Freeman Mbowe ya kuomba kukutana na Rais Samia.
Rais amekubali kukutana na kushauriana na Chadema, tunasubiri kujulishwa tarehe
ya kukutana.”
Hatua ya Rais Samia kukubali ombi la Chadema limekuja siku chache baada ya kuhutubia
Bunge na kueleza kuwa anakusudia kukutana na viongozi wa vyama vya siasa
Tanzania ili kuweka mwelekeo wa kuendesha shughuli za siasa zenye tija na
maslahi kwa nchi.
“Katika kulinda uhuru wa kidemokrasia nakusudia kukutana na viongozi wa vyama
vya siasa Tanzania ili kwa pamoja tuweke mwelekeo wa kuendesha shughuli za
siasa zenye tija na maslahi kwa ajili ya nchi yetu,” alisema Rais Samia.
Katibu Mkuu
wa Chadema, John Mnyika amesema ombi lao la kukutana na Rais Samia Suluhu
Hassan limekubaliwa na wakati wowote watakutana na kiongozi huyo.
No comments:
Post a Comment