Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Halima Mdee na wenzake 18 wamevuliwa uanachama wa chama hicho kwa sababu wamekiuka katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum bila chama hicho kuwapitisha.
Mbowe ametoa tamko hilo leo Ijumaa Novemba 27, 2020 saa
5 usiku wakati akisoma maazimio ya kikao cha kamati kuu kilichoketi kuanzia saa
3 asubuhi kuwajadili wabunge hao.
Waliovuliwa uanachama ni Halima Mdee, Esther
Matiko, Grace Tendega, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta
Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo,
Asia Mohammed, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti
Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta
Rwamlaza.
Kabla ya kutangaza uamuzi huo, Mbowe alitaja hatua
nyingine tatu ambazo kamati kuu imezichukua ikiwa ni pamoja na kuwavua
nyadhifa miongoni mwao waliokuwa viongozi wa Baraza la Vijana la chama hicho
(Bavicha) na lile la wanawake (Bawacha) na kuagiza mchakato wa kujaza nafasi
zao uanze mara moja.
“Tumeagiza kurugenzi yetu ya kisheria itafute taratibu
mbalimbali za kisheria kupinga mchakato wa kuwapata wabunge 19 wa Chadema kwa
sababu mchakato huo ni batili kuanzia hatua ya mwanzo maana wameghushi majina
na waliopelekewa majina nao wameyapokea,” alisema Mbowe.
Mbowe amesema licha ya kuwaita kuhojiwa hawakutokea huku
wakitoa sababu zinazofanana kwamba waongezewe siku saba wajitafakari kwa madai
wanahofia usalama wao kwa madai kuwa kuna wanachama walijipanga kuwafanyia vurugu.
Mwenyekiti huyo wa Chadema amesema wana nafasi ya kuomba radhi ili kurejeshewa
uanachama wao na kama hawakuridhika na uamuzi huo wana haki ya kukata rufaa.
“Kikao cha kamati kuu hakikufanyika makao makuu ya chama tulikifanya
katika hoteli ya Ledger Plaza (zamani Bahari Beach) Ili kuhakikisha wanakuwa
huru zaidi ila wao hawakuja wote na pia tuliwapigia simu kusisitiza waje, hawa
dada zetu wamekumbwa na nini,” amesema Mbowe.
No comments:
Post a Comment