Hatimaye klabu ya Liverpool itakabidhiwa kombe
la ligi kuu ya England EPL leo usiku kwenye mchezo wao dhidi ya Chelsea katika
dimba la Anfield ukiwa ni mchezo wao wa mwisho katika uwanja wao wa nyumbani
msimu huu.
Ni ubingwa wa kwanza wa EPL kwa Liverpool baada ya kipindi
cha takribani miaka 30 na ni kwa mara ya kwanza wanatwaa taji hili la ligi kuu
yani premier League.
Mara ya mwisho majogoo hao wa jiji kuchukua taji la ligi
ilikua mwaka 1990 ambapo mashindano yalikua katika mfumo wa daraja la kwanza
yani first Divison, kabla ya mfumo kubadilika mwaka 1992 na kuwa Ligi kuu.
Jordan Harnderson ,nahodha wa kwanza wa Liverpool
atakayeingia kwenye vitabu vya kumbukumbu na ndie atakae kabidhiwa kombe hilo
na anakuwa nahodha wa 10 katika historia ya Liverpool kufanya hivyo.
Manahodha waliowahi kunyanyua makwapa kwa kubeba taji la
ligi wakiwa na Liverpool ni Graeme Souness, Phil Thompson, Emlyn Hughes, Tommy
Smith, Ron Yeats, Willie Fagan, Donald McKinlay na Alex Raisbeck .
Licha ya kupita vizazi vyenye vipaji vya aina yake,kama
nahodha Steven Gerlad,Jammie Callagher,Michae Owen,Robbie Fowler ,David
Ginola,Luis Suarez,Sammi Hypia,Milan Baros ,hao ni baadhi tu ,lakini EPL ilikua
mtihani uliowashinda kabisa.
Makocha bora wakiwemo akina Rafael Benitez enzi hizo,Brendan
Rodgers, lakini Liverpool iliishia kutwaa mataji mengine,lakini hili la EPL
ilishindikana.
Ndio maana Jurgen Klopp atapata heshima kubwa kutoka kwa
mashabiki wa Liverpool popote duniani kutokana na kurejesha heshima yao
iliyopoteza kwa takribani miaka 30 iliyopita.
Liverpool watatamani kukabidhiwa ubingwa huo kwa matokeo ya
ushindi dhidi ya Chelsea ambao waliipa ubingwa Liverpool zikiwa zimebaki mechi
saba baada kabla ya ligi kumalizika kwa kuifunga Manchester city ambao walikuwa
wapinzani wa karibu wa Liverpool kwenye mbio za ubingwa.
Lakini Chelsea nao wanamahitaji makubwa ya alama zote 3
kuliko sherehe za ubibngwa za Liverpool kwani wao bado wapo kwenye vita ya
kupambana kualiza katika nafasi 4 za juu ili kujihakikishia nafasi ya kucheza
klabu bingwa ulaya msimu ujao.
Chelsea wapo nafasi ya 3 kwenye msimamo na alama zao 63
ikiwa ni tofauti ya alama 1 tu na Lecester city na Manchester United walio
nafasi ya 4 na 5 ambapo mashetani wekundu usiku huu wapo kibaruani kuikabili
West Ham United.
Msimu huu Liverpool hawajapoteza mchezo katika uwanja wao wa
kwenye EPL katika michezo 18 wameshinda michezo 17 na wamesare mchezo 1.
No comments:
Post a Comment