Hatma ya kufunguliwa kwa Shule na vyuo Uganda kuamuliwa kabla ya Septemba,Makanisa na misikiti kuendelea kufungwa.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni
ametangaza kwamba ni mapema sana kuruhusu shule na vyuo kufunguliwa au
kufutilia mbali kabisa kwa kalenda ya masomo mwaka huu,akiahidi kutoa mwelekeo
kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.
Shule na vyuo ni miongoni mwa sekta
za kwanza kuathirika na marufuku ya kudhibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.
Museveni anasema kwamba mpango wa
kuwapa wanafunzi redio ili kuendelea na masomo ya kidijitali unaendelea,akiwa
amwemwagiza waziri wa Elimu ambaye ni mkewe Janeth Museveni na waziri wa fedha
kusimamia zoezi hilo.
Kando na Elimu Museveni amesema
kwamba makanisa na misikiti itaendelea kufungwa hadi pale mbinu mwafaka ya
kuyaruhusu kuendelea na Ibaada itabuniwa.
Marufuku ya kutotoka nje usiku
imesongeshwa hadi saa tatu Usiku kutoka saa moja Jioni.
Majengo ya kibiashara maarufu
Arcades 110,Maeneo ya vinyozi na kushuka nyweli yameruhusiwa kufunguliwa japo
chini ya masharti ya kunakili majina na namba za vitambulisho na za simu za
wateja,kuvalia barakoa,kuosha mikono miongoni mwa masharti mengine
yaliyotangazwa awali.
Safari za ndege na mipaka itaendelea
kufungwa.
Safari za pikipiki maarufu boda boda
zitarejelewa kuanzia julai 27,wahudumu na wateja wakitakiwa kuzingatia masharti
ya wizara ya afya,ikiwemo kunakili stakabadhi za wateja.
No comments:
Post a Comment