Walimu 2 wa Sekondari Wilayani
Iramba, Singida wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kwa kukutwa na hatia ya
kumbaka kwa zamu Mwanafunzi wao wa kidato cha pili(15),
Waliohukumiwa ni Ernest Emmanuel
(25) na Onesmo Bida (28), huku wenzao wawili ambao pia wanatuhumiwa kumbaka
mwanafunzi huyo, kesi yao bado inaendelea.
Walimu hao wanne, wanadaiwa kumbaka
mwanafunzi huyo kwa zamu huku wakijua kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria
namba 130 kifungu (1) kifungu kidogo (2) (E) kilichofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali,
Lyoba Mkambala, alidai mahakamani hapo mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya
Iramba, Makwaya Charles, kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo kwa nyakati
tofauti toka Machi 2 mwaka jana hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Mkambala alidai mshtakiwa Ernest
Emmanuel, alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na dada wa mwanafunzi huyo.
Alidai Machi 20 mwaka jana, saa 2
usiku, mwanafunzi huyo alienda nyumbani kwa shemeji yake Emmanuel kwa lengo la
kuangalia sinema (movie).
“Baada ya kumaliza kuangalia
‘movie’, mwanafunzi huyo aliamua kurejea kwenye nyumba ambayo alikuwa amepanga.
Mwalimu Emmanuel aliamua kumsindikiza na kuingia naye chumbani.
“Mwanafunzi alimbebeleza mwalimu
wake ambaye pia ni shemeji yake arudi kwake ili yeye aweze kujisomea, lakini
mwalimu alikataa na kisha kumshika kwa nguvu na kumwingilia kimwili,” alidai
Mkambala.
Alidai kuwa Januari 21, mwaka huu,
wazazi wa mwanafunzi huyo walimchukua binti yao na kwenda naye hadi kwa mkuu wa
shule kushtaki kwamba mtoto wao anakataa shule.
“Mwanafunzi huyo baada ya kuhojiwa,
alisema ana mimba. Pia alitumia nafasi hiyo kutaja walimu waliomwingilia
kimwili kuwa ni Ernest Emmanuel, Onesmo Bida, Keneth Komba na Ally Pangu,
aliosema kila mmoja alimbaka kwa muda wake,” alidai.
Walimu wawili jela miaka 30 kwa kumbaka mwanafunzi kwa zamu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
September 08, 2019
Rating:
No comments:
Post a Comment