Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ametoa siku 30 kwa kampuni ya
simu ya Vodacom kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)
kutoa suluhisho la wizi wa mtandao kwa wateja wake
Kamwelwe alitoa
agizo hilo jana alipotembelea ofisi za TCRA ikiwa ni mara ya kwanza tangu
alipohamishiwa wizara hiyo Julai mosi katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri
yaliyofanywa na Rais John Magufuli.
Katika ziara TCRA, waziri alishuhudia
makabidhiano ya leseni ya masafa ya 700MHZ kwa kampuni ya Vodacom
Waziri alisema
ni lazima Vodacom kwa kushirikiana na TCRA wakae na kutafakari suala la wizi wa
fedha kwenye laini za simu kwa kuwa wao ndio wanaotakiwa kufahamu ni kwa nini
wateja wanaibiwa
Kamwelwe
alisema kabla hawajaweka sheria itakayowalazimu kurudisha fedha za mteja
itakayoibwa, lazima wakae kuangalia watu hao kama ni wafanyakazi waliofukuzwa
Naye
mkurugenzi mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema ili kuhakikisha malengo na faida
za mnada zinafikiwa wameweka masharti yanayotakiwa kufuatwa.
Wizi muda wa maongezi wamkera waziri
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment