Polisi wilayani Serengeti Mkoa wa Mara wanawashikiria watu
kumi kwa kosa la kukutwa na nyara za Taifa kinyume cha sheria
Kamanda wa Polisi mkoa huo, Juma Ndaki akizungumza na
waandishi leo Jumapili Julai 22, 2018 amesema watuhumiwa hao wamekutwa na
vipande 531 vya nyama kavu, mikia 24 ya nyumbu, mikia 12 ya pundamilia, nyaya
75 za kutegea, mapanga mawili, visu viwili, dumu nane za maji na baiskeli
10
Ndaki amesema mzigo huo ulilkamatwa kwenye kambi yao ya ujangili
eneo la Togoro ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa
ushirikiano wa askari wa Hifadhi hiyo na Polisi wilayani humo
Amesema kuwa Watuhumiwa wote ni wakazi wa kata za Nyambureti
na Nyamatare wilayani Serengeti
Watu 10 mbaroni kwa kukutwa na nyara za Taifa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment