BARAZA la Wafugaji Ngorongoro, limeziondoa hofu kampuni za
wawekezaji wanaoonyesha nia ya kuwekeza katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
(NCAA), kuwa watapokelewa na kushirikiana nao
Hatua ya Maura kutoa ukaribisho wa kushirikiana na wawezaji
hao ilifuatia hofu iliyoonyeshwa na baadhi ya wawekezaji kuhusu uwepo wao
katika eneo hilo
Kwa mujibu wa sheria, NCAA ni hifadhi ambayo inaruhusu uwepo
wa makazi ya binadamu na mifugo
Akizungumza katika mkutano huo, Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Japhet Hasunga, alisema baadhi ya maeneo ya uwekezaji wa kitalii
yamekuwa na matatizo na wawekezaji isipokuwa NCAA
“Baraza limesema hapa, wapo tayari kushirikiana pamoja na
wawekezaji,” alisema
Aliwapongeza NCAA kuwaleta pamoja wawekezaji na kuwaonyesha
fursa au maeneo ya uwekezaji ambayo yataongeza idadi ya watalii hadi kufikia
milioni mbili kwa mujibu wa matarajio ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020
Hivi karibuni, Rais John Magufuli alisisitiza umuhimu wa
sekta ya utalii kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini
Kwa upande wake, Naibu Mhifadhi Mkuu wa NCAA, Dk. Maurus
Msuha, alielezea umuhimu wa kuwekeza katika maeneo ya vivutio vilivyopo ili
kuwashawishi watalii kutumia siku nyingi kukaa kutembelea vivutio hivyo badala
ya siku moja au mbili
Naye Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Rashid Taka,
aliwahamasisha wananchi kushiriki kwa wingi kikamilifu katika uwekezaji.
Alisema jamii inayowazunguka inategemea kunufaika
na mapato ya uwekezaji huo
Mapema wiki iliyopita, wawekezaji hao walitembelea maeneo
mbalimbali ya vivutio vilivyopo NCAA kwa lengo la kuainisha aina ya uwekezaji
unaofaa
Maeneo waliyotembelea ni OIduvai kwa ujenzi wa kiwanja cha
ndege, kituo cha mafuta, Makumbusho ya masalia ya Zamadamu na zana zake
yaliyopo Olduvai Gorge, kituo cha jamii cha Olduvai kwa ajili ya shughuli za
kitamaduni, jengo la chakula, eneo la Laetoli ambako nyayo za binadamu wa kale
ziligunduliwa
Sehemu zingine ni kreta hususani, katika banda maalum ambalo
limejengwa kwa ajili ya kumtunza faru Fausta ambaye ni mzee wa umri wa miaka
55, sasa na mtoto wa simba ambaye amefanyiwa upasuaji mara kadhaa
Wafugaji Ngorongoro wakaribisha wawekezaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment