Mrema amfagilia Lugola, asema anaweza kuvaa viatu vyake


Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema amefagilia utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akibainisha kuwa ameanza na kasi nzuri

Amesema Lugola akiendelea na kasi hiyo ataweza kuvaa viatu vyake alipokuwa waziri  wa wizara hiyo wakati wa utawala  wa Serikali ya Awamu ya Pili

Mwenyekiti huyo wa bodi ya Taifa ya Parole na mbunge wa zamani wa Vunjo ametoa kauli hiyo leo  Ijumaa Julai 27, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini hapa

“Lugola ameanza vizuri amenifurahisha pale aliposema kuwa atahakikisha anadhibiti watu kubambikiziwa kesi na baadhi ya askari wasio waaminifu,"amesema Mrema

Amesema wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, watu walimchukia kutokana na utendaji kazi wake ikiwa ni pamoja na kuwakamata watumishi wa Serikali waliokiuka utaratibu na kufanya makosa.

 “Nilisema wizara zote zangu na aliyefanya kosa alikamatwa. Nilikuwa kero kwa baadhi ya watu, lakini sikujali  na hicho ndio anakifanya Lugola kwa sasa, nampongeza kwa hilo,” amesema

Amesema yupo tayari kumwonyesha Lugola kile alichokiita vichochoro alivyovipitia katika utendaji kazi wake wa wakati huo ili vimsaidie waziri huyo katika  utekelezaji wa majukumu yake

Mrema amfagilia Lugola, asema anaweza kuvaa viatu vyake Mrema amfagilia Lugola, asema anaweza kuvaa viatu vyake Reviewed by KUSAGANEWS on July 27, 2018 Rating: 5

No comments: