Mkurugenzi wa halmashauri ya Arusha Dc Dkt Charles
Mahera amesema wamefanikiwa kuhamisha mnada wa Soko la mifugo ngaramtoni kwenda
eneo la Lengijave katika kata ya Olkokola ambapo mnada huo una miundombinu ya
kutosha kwa wafanyabiashara.
Akiwa katika eneo hilo na wananchi Dkt Mahera amesema
kuwa mnada huo ulikuwepo tangu mwaka 1962 na mwaka 2007 miundombinu ikajengwa
na vikao vilishakaa kukubaliana mnada huo utumike lakini baadhi ya watu
waliokuwa na maslahi binafsi wakalazimisha mnada huo kuwa Ngaramtoni.
Amesema kuwa hayo yamefanyika kwasababu eneo la awali
Ngaramtoni ni mamlaka ya mji mdogo hivyo eneo ni dogo ukilinganisha na idadi ya
wafanyabiashara wanaofika mnadani ambapo lengo la halmashauri ni kwa ajili ya
kuboresha hali ya wafanyabiashara ili kuongeza kipato.
Dkt Mahera Ameongeza kuwa eneo hilo liko nje kabisa ya
mji hivyo linatoa pia fursa kwa halmashauri kuongeza mapato tofauti na
ilivyokuwa mwanzo kwasababu idadi ya watu inaongezeka na soko hilo ni kila siku
ya alhamisi na jumapili.
Kwa upande wa Diwani wa kata ya Olkokola Mh Kalanga
Laizer amesema kuwa awali mnada huo ulinanza kutumika mwaka 1962 hivyo
halmashauri ya Arusha Dc ikaanza kufufua upya kutokana na migogoro ambayo haina
maana baina yao.
Akizungumzia fursa zitakazopatikana kwenye mnada huo
ambao unaingiza zaidi ya watu elfu moja amesema kuwa kutakuwa na mamantilie wa
kutosha,pamoja na halmashauri ujenga vibanda ili kukodisha kwa wafanyabiashara
pamoja na ajira kwa watu mbalimbali ikiwemo usafi kwenye eneo hilo la mnada.
Nao wafanyabiashara katika mnada huo wameiomba
halmashauri kuwajengea ukuta wa kuzunguuka kwasababu ya eneo hilo kuwa na
baridi pamoja na upepo mkali jambo litakalowasaidia hata afya zao.
Mkurugenzi Arusha Dc Dkt Mahera awahamishia wafanyabiashara wa Mifugo kwenye mnada wa Kisasa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment