Dakika 60 za
hukumu ya kifo kwa washtakiwa watano wa mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa
Mirerani na Arusha, Erasto Msuya, jana zilihitimisha kesi ya mauaji ya
kukusudia iliyochukua miaka mitatu
Hukumu hiyo
imetoka wakati kesi ya Miriam Mrita, ambaye n
i mke wa marehemu Msuya, ikitajwa
jijini Dar es Salaam. Miriam ameshtakiwa kwa tuhuma za kumuua dada wa mumewe
ambaye ni maarufu kwa jina la Bilionea Msuya
Jijini Moshi,
baada ya hukumu kusomwa, ndugu wa Bilionea Msuya akiwemo dada yake anayeitwa
Antuja walijikuta wakibubujikwa machozi, huku wakiishukuru mahakama kwa maelezo
kuwa imetenda haki
Msuya
aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa jijini Arusha, aliuawa kwa kupigwa
risasi na bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7, 2013 eneo la
Mijohoroni wilayani Hai
Katika eneo la
tukio kuliokotwa maganda ya risasi za SMG 22 ambako pia lilikutwa gari lake
aina ya Range Rover namba T800 CKF, bastola zake na simu zake mbili
Katika hukumu
iliyosomwa na Jaji Salma Maghimbi kuanzia saa 3:40 asubuhi hadi saa 4:40
asubuhi Mahakama Kuu iliwahukumu adhabu ya kifo washtakiwa watano na kumuachia
huru mmoja
Waliohukumiwa
kunyongwa ni Sharif Mohamed ambaye ni mshtakiwa wa kwanza, Mussa Mangu
(mshtakiwa wa tatu), Karimu Kihundwa (wa tano), (Sadik Jabir (wa sita) na Ally
Majeshi ambaye ni mshtakiwa wa wa saba
Jaji Maghimbi
alimuachia huru mshtakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne, maarufu kwa jina la Mredii
kutokana na kukosekana ushahidi dhidi yake
Akichambua
ushahidi dhidi ya washtakiwa hao, Jaji Maghimbi alisema mahakama imezingatia
maelezo ya kukiri kosa na ya ungamo la washtakiwa wanne na pia ushahidi huru
kuunga mkono
Maelezo ya
kukiri kosa ambayo yalipokewa na kusomwa mahakamani yalihusu mpango mzima wa
mauaji hayo na ushiriki wa Sharifu, Mangu, Karim, Sadick na Ally Majeshi
Kwa mujibu wa
Jaji Maghimbi, maelezo ya Sharifu ambayo yaliungwa mkono na mashahidi wengine
wa upande wa mashtaka, yanaeleza mpango mzima wa mauaji ulivyosukwa na bunduki
ya SMG ilivyonunuliwa
Pia katika
maelezo hayo, mshtakiwa huyo alieleza namna laini mpya za simu zilivyosajiliwa
kwa majina ya Kimasai na namna pikipiki mbili zilizotumika katika mauaji hayo,
zilivyonunuliwa
Kuhusu
mshtakiwa wa tatu, Jaji Maghimbi alisema ingawa katika maelezo yake ya kukiri
kosa alianza kwa kujitoa na kuwabebesha mzigo washtakiwa wenzake, alishiriki
katika nia hiyo ovu
“Alijua mpango
huo wa mauaji na akaendelea kushiriki katika mipango hiyo ya mauaji hadi mwisho
bila kujitoa,” alisema Jaji
“Kitendo cha
kutojitoa katika mpango mzima wa mauaji kinaonyesha nia yake ovu ya kutenda
kosa hilo. Hakufanya juhudi zozote za kujitoa katika mipango hiyo miovu ya
mauaji,” alisema Jaji
Jaji Maghimbi
alisema maelezo ya Karim aliyeeleza kuwa ndiye aliyemfyatulia risasi nyingi
Msuya, yanaunganika na yake waliyoeleza Sharifu, Mussa na Majeshi
Jaji Maghimbi
alisema maelezo hayo ya kukiri kosa na maungamo ya washtakiwa, yaliungwa mkono
na mashahidi wengine wa Jamhuri na hivyo kuthibitisha shtaka la mauaji pasipo
kuacha shaka yoyote
Katika kesi
hiyo, upande wa mashtaka ulioongozwa na wakili mwandamizi wa Serikali, Abdalah
Chavulla uliita mashahidi 27 waliotoa ushahidi kwa kuongea na watano ambao
maelezo yao yalisomwa
Chavulla
ambaye alisaidiana na wakili mwandamizi wa Serikali, Omary Kibwana na mawakili
Ignas Mwinuka, Kassim Nassir na Lucy Kyusa pia waliwasilisha vidhibiti 26 vya
kesi hiyo
Kabla ya
kutolewa kwa adhabu, wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama
izingatie umri mdogo walionao washtakiwa na kwamba wamekaa muda mrefu gerezani
na wanajutia kosa hilo
‘Nimemuona
Mungu’Hukumu hiyo ilikuwa habari njema kwa ndugu wa Bilionea Msuya
“Kwa kweli
katika jambo hili nimemuona Mungu akitenda haki,” alisema Antuja Msuya, ambaye
ni dada wa Bilionea Msuya
“Nawashukuru
wapelelezi makini waliopeleleza kesi hii. Zaidi ya yote namshukuru jaji
aliyetoa hukumu hii
“Kama familia
nasema asante na tumeridhishwa na uamuzi huu.”
Antuja, huku
akimiminika machozi na akibembelezwa na wenzake alishindwa kuendelea kuzungumza
Baba mzazi wa
marehemu, Simon Msuya pia aliishukuru mahakama, lakini akasema hakuridhishwa na
hatua ya jaji kumuachia huru mshtakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne
Jijini Dar es
Salaam, jalada la kesi ya mauaji inayomkabili Miriam Mrita, sasa lipo kwa
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
Wakili wa
Serikali, Patrick Mwita alisema mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa
jalada hilo linafanyiwa kazi na DPP
Wakili wa
upande wa utetezi, Peter Kibatala aliutaka upande wa mashtaka ufuatilie jalada
hilo kwa kuwa sasa liko mikononi mwa DPP
Katika kesi
hiyo ambayo imeahirishwa hadi Julai 30, washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa
makusudi Aneth Msuya, ambaye ni dada wa Bilionea Msuya, Mei 25, 2016 Kigamboni
jijini Dar es Salaam
Mtiririko
matukio ya kesi
Agosti 7,2013 Bilionea Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi
sehemu mbalimbali za mwili eneo la Mjohoroni wilayani Hai
Polisi
inatangaza kukamatwa kwa washukiwa muhimu wakihusishwa na mtandao uliofanya
mauaji hayo
Agosti 21,2013
Watuhumiwa
watatu, Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne na Mussa Mangu wanafikishwa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Moshi kujibu shtala la kumuua kwa makusudi Msuya
Septemba 16,
2013
Kamanda wa
Polisi Kilimanjaro wa wakati huo, Robert Boaz anatangaza kukamatwa kwa
watuhumiwa wanne zaidi. Watuhumiwa hao ni Joseph Mwakipesile au Chusa
(mfanyabiashara tajiri wa Mirerani), Sadick Mohamed, Karim Kihundwa na Jalila
Said
Septemba 18,
2013
Mwakipesile,
Mohamed, Kihundwa na Said wanafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji hayo
Aprili 16,
2014
DPP anamfutia
mashtaka Mwakipesile, akitumia kifungu na. 91 cha sheria ya mwenendo wa
mashauri ya Jinai (CPA) ya 2002
Juni 10, 2014
Upande wa
mashtaka unawasomea washtakiwa maelezo ya mashahidi 50 wa kesi hiyo na kutaja
vielelezo vitakavyotumika.
Februari 10, 2015
Washtakiwa
wanasomewa shtaka la mauaji ya kukusudia mbele ya Jaji Amaisario Munisi na wanakana
kumuua Bilionea Msuya.
Oktoba 5, 2015
Kesi ya
Bilionea Msuya inaanza kusikilizwa na Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu.
Mei 14, 2018
Jaji Maghimbi
anamuachia huru mshtakiwa wa nne, Jalila Zuber baada ya kumuona hana hatia
kulingana na ushahidi wa watu 32 wa mashtaka na vielelezo 26
Ushahidi wa
upande wa mashtaka
Mashahidi wa
upande wa mashtaka walidai kuwa njama za kumuua Msuya zilianza Julai 2013 na
watuhumiwa waliofanya mauaji waliahidiwa kulipwa Sh17 milioni kila mmoja
lidaiwa kuwa
katika kupanga mauaji hayo, simu mpya tano na laini tano zilisajiliwa kwa
majina ya Kimasai, kununuliwa kwa pikipiki mbili na bunduki aina ya SMG
Katika
ushahidi huo, inadaiwa Majeshi ndiye aliyemvuta Msuya hadi eneo la tukio,
akijifanya anataka kumuuzia madini ya Tanzanite
Kulingana na
maelezo ya ungamo ya Karim na ya onyo la kukiri kosa ya Majeshi, Karim ndiye
aliyemfyatulia risasi mfanyabiashara huyo
Katika
ushahidi wake, Dk Paul Chaote aliyeufanyia uchunguzi mwili wa Msuya alidai
ulikuwa na majeraha 26 ya risasi yaliyosababisha mfumo wa damu na upumuaji
kusimama
Dk Chaote
alidai kwa kuutazama kwa nje, mwili wa marehemu ulikuwa na majeraha madogo 13
na makubwa 13 yaliyosababishwa na risasi zilizoingia mwilini na kutokea upande
wa pili
Alidai baada
ya kuupasua mwili wa marehemu, walikuta utumbo mwembamba umekatika huku risasi
hizo zikiharibu figo, mishipa ya damu na kupasua bandama
Dk Chaote
alidai mapafu yote mawili yaliharibiwa vibaya kwa risasi huku mishipa ya damu
inayoingia kwenye mapafu, figo na bandama ikiwa imechakazwa vibaya kwa risasi
Katika
ushahidi wao, mashahidi wote waliegemea katika ushahidi wa mazingira ambao
maofisa wa polisi walieleza namna washtakiwa walivyoshiriki tukio hilo na namna
walivyowakamata
Nyongeza na
Tausi Ally, Dar es Salaam
Jaji atumia dakika 60 kuwahukumu kifo watu watano kesi ya Msuya
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment