Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Manyara
kimewapitisha wagombea watano wa udiwani watakaopeperusha bendera ya chama
hicho katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu
Akizungumza na Mwananchi katibu wa chama hicho Mkoa wa
Manyara, Gervas Sulle alisema chama hicho kimejipanga kushinda uchaguzi wa kata
hizo
Alisema chama hicho kitamsimamisha Mathias Zebedayo kugombea
udiwani Kata ya Bagara mjini Babati
Wagombea wengine ni Theophil Lolo wa Kata ya Masakta,
Philipo Mallo (Gehandu), Zacharia Nihhi Tumati na Daniel Boa, Hayderer
Alisema chama hicho kimejipanga kushinda kata hizo kwa
kufanya kampeni za kistaarabu kwa kuuza hoja zao na kwamba endapo uchaguzi
utakuwa wa huru na wa haki, wataibuka na ushindi.
“Kwenye kata nne kati ya tano, Chadema ilikuwa inaongoza
udiwani, tunatarajia wananchi wa Manyara watawachagua tena wagombea wetu na
kushinda upya uchaguzi huo mapema sana,” alisema Sulle
Mbunge wa Babati Mjini (Chadema), Pauline Gekul alisema
wananchi ndiyo watakaoamua kwa ridhaa yao kwa kumchagua mgombea udiwani mwenye
uwezo wa kutetea masilahi yao
“Chadema kwenye mikutano yetu ya ndani tumepanga mikakati;
kesho (leo) tutaanza kampeni ya kumnadi mgombea udiwani Kata ya Bagara Mjini
Babati, kwani awali ilikuwa kata yetu,” alisema Gekul
Uchaguzi katika kata hizo unafanyika kufuatia madiwani wanne
wa Chadema na mmoja wa ACT-Wazalendo kujiuzulu na kuhamia CCM kwa maelezo kuwa
wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli
Katika mchakato wa kura ya maoni ndani ya chama hicho
tawala, CCM imewapitisha tena wagombea hao waliokuwa madiwani wa Chadema na
ACT, kuwania udiwani.
Uchaguzi wa kata 79
na Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma umepangwa kufanyika Agosti 12
Chadema wapitisha wagombea watano wa udiwani Manyara
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment