Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema watakaobainika
kuhusika na madudu yaliyomo katika taarifa za kamati maalum za Bunge
zilizoundwa kuchanguza masuala ya gesi asilia na uvuvi wa bahari kuu,
watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani
“Kuna
watuhumiwa wawili wametajwa, vyombo vya dola vinatakiwa kuchukua hatua kwa wale
walioghushi lesini za uvuvi,” amesema Mbarawa leo Juni 2, 2018 katika hafla ya
kamati hizo zilizoundwa na Spika Job Ndugai, kukabidhi taarifa zake za
uchunguzi kuhusu maeneo hayo mawili iliyofanyika viwanja vya Bunge mjini Dodoma
Mbarawa ambaye
amemuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, “Tumeyasikia mengi,
Watanzania wamesikia mengi kuhusu ripoti hizi. Tutasoma ripoti hizi neno kwa
neno, mstari kwa mstari na kipengele kwa kipengele. Niwahakikishe Bunge na
Watanzania kwamba mapendekezo tutayatekeleza kwa haraka.”
“Kuna shida
katika mikataba hasa gesi asilia. Utasikia kuna kasoro katika mikataba na
Serikali ya Awamu ya Tano tumelisikia na tumejipanga na tutafanyia kazi. Kama
ambavyo ripoti zimeeleza, wale ambao walihusika tutafanya uchunguzi na sheria
itachukua mkono wake.”
Amesema katika
sekta ya uvuvi kuna shida ya sera, kanuni ,sheria na kuahidi kuzifanyia kazi
ili uvuvi uwe na maslahi kwa Taifa.<
Waliotajwa katika taarifa za Bunge kuburuzwa mahakamani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment