|
Dodoma. Spika Job Ndugai leo
amelazimika kumpokonya Najma Giga uongozi wa kikao cha Bunge baada ya mzozo
uliosababishwa na mbunge wa CCM aliyewafananisha wapinzani na mbwa
Spika Ndugai alifanya kitendo
hicho kisicho cha kawaida katika kikao cha 44 cha Mkutano wa Kumi na Moja wa
Bunge wakati wa kujadili hotuba ya bajeti ya mwaka 2018/19 ya Wizara ya Fedha
na Mipango
Wakati akichangia, mbunge huyo wa
Jang’ombe, Ali Omar alisema: “Ukiona majuha wanapongezana wakaona wamefanya
la maana, kuna hawa mbwa kama tutawatoa itakuwa vizuri sana. Nasikia milio ya
mbwa ukiwatoa itakuwa vizuri.”
Baada ya kauli hiyo, wabunge
wawili kutoka Chadema, Joseph Selasini (Rombo) na Mchungaji Peter Msigwa
(Iringa Mjini) walisimama kutaka utaratibu ufuatwe kwa mchangiaji kuomba
radhi
Hata hivyo, Giga hakuruhusu hilo
na kusababisha wabunge wengine wa upinzani kupiga kelele wakimtaka mbunge
huyo afute kauli hiyo
Giga alitumia kama dakika mbili
kuwazuia lakini hakuweza na kumtaka Omar aendelee kuchangia
Hata hivyo hakuweza kuwazuia
kutokana na wabunge hao wa upinzani kuendelea kupiga kelele wakisisitiza Omar
ashinikizwe kufuta kauli yake.
Wakati kelele zikiendelea na utulivu
bungeni ukitoweka, Spika Ndugai akaingia na kuchukua uongozi wa kikao na
hivyo Giga, aliyeanza kuongoza kikao hicho tangu asubuhi, kulazimika
kumuachia uongozi
|
|
Spika Ndugai ‘ampokonya’ mwenyekiti uongozi baada ya wapinzani kuitwa mbwa
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 05, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment