Pacha wa
kipekee wa Tanzania walioungana, Maria na Consolata Mwakikuti wamefariki dunia
usiku wa leo (Jumamosi, June 2) katika hospitali ya mkoa ya Iringa
Taarifa
zilizoifikia Mwananchi Digital na kuthibitishwa na mkuu wa wilaya wa Iringa
Richard Kasesela, zimebainisha kuwa mapacha hao wamefariki wakipishana kwa
takribani saa 2
"Wamepigania
sana afya zao, mida ya saa moja hivi jioni ndio nimepokea taarifa za kifo chao
na kwa sababu nilikuwa mazingira ya hospitali basi nilisogea kuwaona – na ni
kweli hatunao,” amesema Kasesela
Tanzia toka
hospitali inaonyesha pacha wa kwanza alifariki majira ya saa 1 usiku, huku mwenzake
akifariki saa 3 usiku
"Kwa hiyo
taarifa zaidi na nini kinaendelea kesho tutakipata. Mungu awapumzishe pema
peponi, Amina.”
Mapacha hao
wamekuwa na historia ya matatizo ya moyo. Tangu Disemba 2017 pacha hao walianza
kuumwa na kulazwa hospitali ya mkoa ya Iringa
Baadaye
walihamishiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili, walipolazwa kwa takribani miezi miwili kwa ajili ya
matibabu mpaka waliporuhusiwa kurejea tena Iringa mnamo Mei 17
Maria na
Consolata walizaliwa wilayani Makete mkoani Njombe mwaka 1996.
Walihitimu
darasa la saba katika shule ya msingi Ikonda, kisha wakajiunga na shule ya
Maria Consolata iliyopo Kilolo mkoani Iringa ambapo walihitimu kidato cha nne
Baada ya hapo,
walijiunga na shule ya Sekondari ya Udzungwa wilani Kilolo walipohitimu kidato
cha sita, ikifuatiwa na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu) walipokuwa
wakisomea fani ya ualimu.
Pacha maarufu walioungana, Maria na Consolata, wafariki dunia
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment