Wanakijiji wa kijiji cha
Remng'orori wilayani Serengeti wamemshtaki Mkuu wa mkoa wa Mara, Adam
Malima kwa Rais John Magufuli kwamba anataka kuwapora ardhi yao wanayotegemea
kwa kilimo na kuwapatia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ili waweke kambi yao.
Baadhi ya wakazi wa kijiji
hicho, wameiambia Nipashe kuwa amri ya Malima imewasababishia ugumu wa maisha
kwa kuwa mwaka huu hawakulima katika ardhi hiyo ambayo ipo mpakani mwa
wilaya za Serengeti na Butiama mkoani Mara.
Mkazi mmoja aliyejitambulisha kwa
jina la Motiba Maro akizungumza na Nipashe amesema, wananchi wa kijiji hicho
wameshindwa cha kufanya kilimo kutokana na amri hiyo ya Malima na kumuomba Rais
Magufuli kuingilia kati.
"Hapa huu mgogoro
umemshinda Malima, lazima Rais atume wasaidizi wake waje wasikilize malalamiko
yetu, ili tupate haki yetu," amesema.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kijiji
cha Remng'orori, Msamba Maro amekiri wananchi wake kuzuiwa kulima katika eneo
hilo, hatua ambayo imewaathiri kwa kuwa mwaka huu watakabiliwa na baa la njaa.
Msamba amesema eneo hilo lina
mgogoro unaohusisha vijiji viwili vya Remng'orori na Mikomariro na mwanzoni mwa
mwaka huu ulisababisha mapigano yaliyosababisha vifo vya watu wawili waliouawa
mwanzoni mwa mwaka huu ulisababisha mapigano yaliyosababisha vifo vya watu
wawili waliouawa kwa kukatwa mapanga.
Mapema mwaka huu Malima akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake, alikiri kwamba mgogoro huo
unasabababishwa na wavamizi kutoka nchi jirani ya Kenya.
Malima ashtakiwa kwa Magufuli
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment