Imeelezwa kuwa shambulio
la aibu kwa mwanamke sio tu kupiga kelele dhidi yake au kumgusa bali hata
kumkonyeza pekee ni lugha ya ishara inayoweza kukupeleka kuenda jela endapo
ushahidi ukithibitika.
Mara baada ya kuibuka mjadala
uliozua gumzo mitandaoni kuhusiana na shambulio la aibu dhidi ya wanawake
eatv.tv ilimtafuta mwanasheria ili kupata ufafanuzi kuhusu shambulio hilo
ambapo, Wakili wakujitegemea Johanes Konda amesema kwamba wanawake wengi
hawatambui kama kukonyezwa bila ridhaa yao ni kosa kisheria.
"Kanuni za adhabu sura ya 16
ndio inaelezea zaidi kuhusiana na shambulio la aibu lakini kulingana na
mazingira na tamaduni zilizopo sasa, dada zetu wanaona kawaida tuu lakini
sheria imewekwa kwa ajili ya kuwatetea wao dhidi ya shambulio hilo ambalo
linaweza kuwa ni kwa kuguswa au kwa ishara kama kukonyeza au kupiga kelele za
kuashiria kuna kitu cha tofauti kimepita", amesema Wakili Konda.
Wakili Konda amesema kuwa endapo
wahusika ambao ni wanawake wakizitambua haki zao na kuwashitaki watuhumiwa
wanaweza kusaidia kuondoa tabia hizo na endapo ikithibitika basi adhabu yake ni
kuanzia miaka isiyozidi 10 kushuka chini.
Hivi karibuni Kamanda wa Polisi wa
mkoa wa mjini Magharibi Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hassan Nassir amesema ni
marufuku kukohoa pale unapopishana au unapomwona mwanamke mwenye makalio
makubwa kwamba kukohoa huko kutapelekea kukamatwa kwa maana kitendo hicho ni
'shambulio la aibu”.
Waweza kwenda jela miaka 5 ukimkonyeza mwanamke
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 17, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment