Mahakama Kuu ya Tanzania imemzuia
Jaji Francis Mutungi na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa nchini au Wakala
wake yeyote yule kutoa fedha za ruzuku za Chama cha Wananchi (CUF), na kumpa
Prof. Ibrahim Lipumba mpaka hapo mashauri ya msingi yanayoendelea Mahakamani
yatakaposikilizwa.
Zuio hilo limetangazwa leo Mei 29,
2018 na Jaji Wilfred Dyansobera katika Mahakama hiyo na kusisitiza kwamba,
maombi ya CUF ya kulinda fedha hizo yana nguvu za kisheria.
Taarifa za chama zinaeleza kuwa hadi
amri hiyo ya Mahakama inatolewa, Jaji Mutungi na Ofisi yake ya Msajili wa Vyama
imeshamruhusu Prof. Lipumba kuchukua zaidi ya shilingi Bilioni 1.5 na fedha
hizo zimekuwa zikiwekwa kwenye akaunti zisizotambuliwa na Bodi Halali ya
Udhamini ya chama na kisha kuhamishiwa kwenye akaunti za watu binafsi akiwemo
Prof. Lipumba Mwenyewe.
Shauri kuhusu uhalali wa Bodi ya
Wadhamini linaendelea kusikilizwa na inatarajiwa kuwa shahidi wa tatu wa upande
wa Chama ataanza kutoa ushahidi wake mwezi Juni mwaka huu.
Mahakama yamzuia Prof. Lipumba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 29, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment