Jamii ya kifugaji imekuwa na imani kuwa suala la
Ukeketaji ni alama inayomtambulisha mwanamke wa jamii hiyo kupata heshima kwa
kuwa anatoka kwenye umri mdogo kwenda utu uzima jambo ambalo mashirika ya
kutetea haki za binadamu imepinga suala hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari wa radio za
jamii,Viongozi wa kimila,Mangariba,waganga wa jadi,viongozi wa dini,pamoja na
maafisa ustawi wa jamii katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Mrakabishi katika jamii ya
kifugaji Bi Susan Koillah amesema ukeketaji umekuwa changamoto kubwa.'
Bi Suzan amesema kuwa kwa jamii hiyo ya kifugaji kwa
mwanamke usipokeketwa unaitwa majina ya udhalilishaji ambayo yanamfanya mhusika
kukata tama ya maisha ya kuishi duniani.
Jamii hiyo ya Kimasai inaamini kuwa mwanamke
asipokeketwa anakuwa na tabia mbaya hivyo wengi hukeketwa kwa kuogopa kutengwa
na jamii na kuogopa kutoolewa hivyo amewataka wanaume kutoamini kwamba mwanamke
aliyekeketwa ndiye anayefaa kuwa mke.
Naye mganga wa jadi katika wilaya ya ngorongoro amesema
kuwa awali alikuwa hafahamu madhara ya ukeketaji lakini kupitia shrikia hi
Kwa upande wa afisa ustawi wa jamii Bwana Benethet
Bwikizo amesema kuwa jamii inatakiwa iingilie kati ili kunusuru tatizo hilo
ikiwemo pia tatizo la watoto kubakwa na kupatwa na Marathi mpaka kufa hivyo ni
wakati wa kuondoa uoga ili kupambana na vitendo hivyo vya kikatili
Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Limeandaa kampeni ya kupinga ukeketaji kwa mwanamke itakayoanza
mwezi wa 6 kwa kuwa ndiyo kipindi ambacho wanafunzi wamefunga shule.
Kamoeni hiyo itashirikisha jamii yenyewe,waganga wa
jadi,waandishi wa habari,wazee wa kimila mangariba na watumishi wa ustawi wa
jamii katika wilaya ya Ngorongoro.
Jamii ya kifugaji inamini kumkeketa mwanamke ni kwa ajili ya kuanza majukumu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 30, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment